SI KWELI Tinashe Jonas atangaza mpango wa kufanya mapinduzi nchini Zimbabwe

SI KWELI Tinashe Jonas atangaza mpango wa kufanya mapinduzi nchini Zimbabwe

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Video ya Kushtua ya Wanajeshi imetolewa ikimuonesha Jonas, wa Kamandi Kuu ya Ideal Zimbabwe, anapinga moja kwa moja serikali ya Zimbabwe na Kuomba msaada wa silaha zaidi katika video yake.

IMG_8414.jpeg

Jonas Alitangaza Mrengo wake mpya wa Kijeshi mwezi uliopita na watu wengi hawakumchukulia kwa uzito wakati huo, ikijumuisha Gambakwe Media.

Mahema na waasi wanaonekana kwa nyuma huku Jonas anazungumza katika kile kinachoonekana kama jumba la kijeshi linalofadhiliwa vyema.


Video ya Tinashe Jonas akizungumza mpango wa kumwondoa madarakani Rais Emmerson Mnangagwa
 
Tunachokijua
Nchi za Afrika zimeendelea kukumbwa na Mapinduzi mfululizo ya Serikali na mengi kati yake yakifanywa na Vikosi vya Kijeshi ambavyo vimekuwa vikitoa sababu mbalimbali ikiwemo kubadili Mifumo isiyoheshimu Utawala Bora.

Tangu mwaka 1952 hadi 2023, kumekuwa na takriban majaribio 214 ya Mapinduzi, 108 yalishindikana, 106 yamefanikiwa. Mataifa 45 kati ya 54 barani Afrika yamepitia wastani wa jaribio moja la mapinduzi tangu 1950.

Katika kipindi cha miaka 3 (2021/23), Nchi 7 (Chad, Mali, Guinea, Sudan, Burkina Faso, Niger na Gabon zimeshuhudia Mapinduzi ya Kijeshi yaliyobadilisha Serikali zilizokuwepo.

Madai ya kuwepo kwa jaribio la mapinduzi nchini Zimbabwe
Kama mwendelezo wa kile kinachotajwa kuwa ni vuguvugu la mapinduzi kwenye nchi za Bara la Afrika, Agosti 27, 2023, video inayotajwa kurekodiwa na mojawapo ya wanajeshi nchini Zimbabwe ilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii hasa TikTok.

Madai haya yaliendelea kusambaa zaidi, na mdau wa JamiiForums mnamo Septemba 4, 2023 alianzisha uzi unaodokeza uwepo wa jambo hili.

Video hii inamuonesha Tinashe Jonas, Mwanaharakati na mpinzani wa kisiasa wa Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akitaja Zaburi 82:3-4, anasema;

"Teteeni wanyonge na yatima,
Tunzeni haki za maskini na walioonewa.
Mwokoeni mnyonge na mhitaji,
Wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu."


Pamoja na mambo mengine, anaendelea kusema kuwa sala bila matendo ni uchawi, na yeye sio mjinga. Akiwa kama Rais wa watu yupo tayari kuwatetea wanyonge dhidi ya Utawala dhalimu wa Rais Emmerson Mnangagwa.

Anafafanua zaidi kuwa Mnangagwa ni shetani, vyombo vyote vya dola pamoja na viongozi wanaoshikilia madaraka makubwa wanatumika kisiasa kumsaidia na kwamba SADC na Umoja wa Afrika wanapaswa kufunga midomo yao, sasa ni wakati muafaka wa kufanya oparesheni ya kijeshi ili kuuondoa utawala ulioko madarakani.

Kweli wa Madai haya upoje?
JamiiForums imefuatilia suala hili na kubaini kuwa video hii ilirekodiwa zamani, Septemba 22, 2019. Uchunguzi wa kimtandao kwa kutumia unathibitisha hili.

Aidha, Septemba 22, 2019, Gazeti la iHarare lilichapisha pia makala inayofafanua tukio hili. Huu ni ushahidi mwingine unaoweka bayana kuwa video hii sio ya sasa.

Jonasi ambaye alikuwa mgombea aliyeshindwa katika uchaguzi wa 2018 anajulikana kwa matamshi yake ya ajabu na aliwahi kutangaza kuwa atawakamata wajumbe wote watatu wa uongozi wa juu nchini humo ikihusisha Rais Emmerson Mnangagwa, Constantino Chiwenga na Kembo Mohadi mnamo 9 Machi 9, 2019 ili wajibu tuhuma mbalimbali.

Wakati huo, Jonasi tayari alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya jinai baada ya kudai kuwa Rais Emmerson Mnangagwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Monica Mutsvangwa, mke wa aliyekuwa Mshauri wake Maalum Christopher Mutsvangwa.

Aliendelea kudai kuwa muungano huo wa uzinzi ulisababisha kuzaliwa kwa mtoto. Baadae alishtakiwa kwa kumtusi na kudhoofisha mamlaka na hadhi ya Rais.
Watu wamevurugwa, hawa wachumia matumbo dawa yao ndio hiyo tu.
 
Back
Top Bottom