GE2025 Tinson Nzunda ajitosa Ubunge Vwawa, achukua fomu CCM Mbozi

GE2025 Tinson Nzunda ajitosa Ubunge Vwawa, achukua fomu CCM Mbozi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Mfanyabiashara na mkulima wa mazao ya Kahawa, Parachichi ,Macadamia na mahindi wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe Tinson Tuloline Nzunda amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Vwawa.

1751264317233.png
Nzunda amekabidhiwa fomu leo June 29,2025 na katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mbozi Julius Mbwiga kwenye ofisi za chama hicho wilaya ya Mbozi zilizopo mjini Vwawa.

Nzunda pia amekuwa diwani wa kata ya Nyimbili wilayani Mbozi kwa kipindi cha miaka kumi kuanzia mwaka 2015 mpaka mwaka huu 2025.

Nzunda amesema licha ya kuchukua fomu hawezi kuzungumza chochote mpaka mchakato wa ndani ya chama juu ya uteuzi wa majina matatu utakapokamilika.

Kwa sasa jimbo la Vwawa linaongozwa na mbunge Japhet Ngailonga Hasunga.
 
Back
Top Bottom