Tinted za kimarekani kwenye gari tunazipenda lakini zinahitaji uvumilivu tu kwakweli

Tinted za kimarekani kwenye gari tunazipenda lakini zinahitaji uvumilivu tu kwakweli

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Tuseme tu ukweli! Ka tinted! ni kaugonjwa ketu wengi!

Sina maana huu uzi niwakuwatambia hapana; siyo lazima niwe na kagari ili kuifurahia tinted, bali hata napopewa lift tu madhila, kero na utamu wa tinted huwa unaonekana!

Tinted ni kilevi kama vilevi vingine visivyolewesha!
Kupenda kunywa Pepsi baridi ni kilevi lakini hakileweshi, kunywa energy drink ni kilevi lakini hakileweshi, kungalia tamthilia ni kilevi lakini hakileweshi, kuangalia mizigo ni kilevi lakini hakileweshi n.k

Kupenda kutumia tinted ni kilevi pia! Ukizoea huwezi kufurahia gari isiyo kuwa na tinted kwani utajiona kama umekaa kibarazani!

Zamani tulizoea kuweka tinted za vioo vya pembeni lakini sasa teknolojia inazidi kukua!
Hivi sasa kuna ingizo jipya almaarufu American tinted!

American tinted wamekuja na tinted ya kioo cha mbele ambacho inadaiwa ukiwa ndani ya gari unaona fresh kabisa!

Mimi ni miongoni mwa watu waliovutiwa kujaribu kuishuhudia American tinted ya kioo cha mbele aina ya 4M!

Ukweli ni kwamba haya ndiyo niliyogundua baada ya kuitumia.
  • American tinted ya kioo cha mbele mchana unaona vizuri kama kawaida lakini usiku inafifia
  • Usiku inahitaji umakini mkubwa kuona vitu ambavyo havina taa au non reflecting object
  • Usiku ukiona mtu anakwenda mbio na tinted ya mbele tambua anatumia uzoefu wa njia (kaikariri njia la sivyo kukiwa na mabadiliko ya njia either ya tuta jipya mbele lazima aliparamie kwa surprise)
  • Kukiwa na mvua au ukungu ni mwendo wa kunyata tu kwaweli
  • Usiku tunazuga hatuna haraka lakini ukweli ni kwamba hatuoni vizuri
  • Kuhama njia kwenye two way traffic boda boda wanatukana sana maana sometimes siyo rahisi kuwaona!
KIUFUPI AMERICAN TINTED YA MBELE IMETAWALIWA NA UVUMILIVU!

Ni nzuri lakini moyoni tunateseka kimya kimya lakini tunavumilia hivyo hivyo!
Tinted ya mbele ni kuvumilia tu!

Siyo kwamba naiponda tinted ya mbele hapana, naipenda lakini starehe yake inahitaji uvumilivu tu katika majira na nyakati!
truck-window-tint.jpg
kilo.jpg
 
Mimi nimeweka tinted za kwenye vioo vya mbele sidhani kama ni American Tinted, ni zile za kukatwa linakuwa kwenye roller na muda wote hata usiku naona vizuri.

Vioo vya kwenye milango nimeweka American tinted zile zinauzwa kwenye viboksi.
 
Tuseme tu ukweli! Ka tinted! ni kaugonjwa ketu wengi!

Sina maana huu uzi niwakuwatambia hapana; siyo lazima niwe na kagari ili kuifurahia tinted, bali hata napopewa lift tu madhila, kero na utamu wa tinted huwa unaonekana!
Hivi kwanini wabongo huwa mnapenda sana kurudia rudia maandishi bila sababu? Inaboa sana.
 
Ni kweli nawashangaaga sana wanaoweka tinted ya kioo cha mbele. Nahisi hata sheria haitaki uweke. Kuna kipindi magari maalumu ndio yalikuwa yanawekewa hiyo tinted. Yaani ukiiona tu unajua gari ya wasiojulikana hiyo.
Kisanga ikifika jioni tu unakaza macho kama unasaka bolt ya saa.
Unatumia nguvu nyingi sana kuona.
Hizi za pembeni tu nikiwa narudi reverse sehemu ya changamoto lazima nishushe vioo ili nipate view nzuri.
 
Hahah kama unasaka nini....wanavumilia tu ili waitendee haki laki ya kubandikiwa
 
Back
Top Bottom