Tips: Jinsi ya kufanya watu/wateja wako kuipenda bidhaa /Huduma yako kwenye Biashara.

Tips: Jinsi ya kufanya watu/wateja wako kuipenda bidhaa /Huduma yako kwenye Biashara.

Makendaa

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2013
Posts
271
Reaction score
141
Kwa nini watu huanza bishara na kushindwa? Tukiangalia tafiti za hivi karibuni, Zinaonyesha kuwa wajasiriamali wengi wameshindwa kuziendeleza Bidhaa zao ambazo zimekuwa zikihitajika na watumiaji kwa kushindwa kuziendeleza . Kuanzisha Biashara ni rahisi ila kuiendeleza hii inahitaji jitihada kubwa ili kuwa na ushindani sokoni. Ndio maana unaona Kampuni kama (Yahoo) mmiliki anataka kuiuza hii ni sababu ya kushindwa kuiendeleza, Au mmiliki / muasisi wa kampuni (mtandao wa kijamii wa Twitter) Kujiuzulu.

CartLove.jpg

Unapo anzisha Bidhaa/huduma ili iweze kukua na kuweza kupambana na washindani inahitajika kuwa na misingi nitakayo ifanya kupendwa na wateja kwa wakati wote.

Kwa mfano halisi, Mjasiriamali mmoja aitwaye Glaxo SmithKline alianza kutengeneza bidhaa ya kupunguza uzito iitwayo Alli. Bidhaa imeweka wazi juu ya madhara yatokanayo na uzito hivyo kukuwekea mkazo kuwa na juhudi katika kuitumia bidhaa hiyo huku ukifanya mazoezi na kukupa matokeo mazuri.


Kwa hiyo unapoitumia ile bidhaa na kuweka juhudi katika mazoezi inakusababisha wewe ndani ya wiki 2 unakuwa umepunguza uzito wa KG2! Hapa moja kwa moja utaona ile bidhaa ina manufaa hivyo kukufanya kuipenda na kutoa ushuhuda kwa wengine na kuifanya kuipenda zaidi. Hivyo watu wanapochagua Bidhaa ya Ali hujiona wamefanya chaguo sahihi litakalo wapa matokeo kwa juhudi zao.

Wengi wetu tumeshindwa kutambua kuwa kuiendeleza bidhaa hufanya bidhaa yako kupendwa na kila mtu na kuifanya kufanya Vizuri sokoni na kuwashinda washindani wako. Si Vizuri tuu kufanya kazi kubwa kuhakikisha wateja wako wanainunua bidhaa yako, Lahasha unatakiwa pia kuhakikisha wateja wako wanaipenda bidhaa yako na kuinunua tena na tena na tena!

Leo hii, watumiaji wengi wa bidhaa ni wadadisi na kutaka kuwa na ufahamu mkubwa wa bidhaa wanayoitumia. Lakini pia hutaka unadhifu wa biadhaa kabla ya kufikia uamuzi wa mwisho wa kununua.

Mfano:

Kitu muhimu mteja anaangalia kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho kununua ni ,Mvuto (mwonekano) gharama, ubora, urahisi, matumizi na usalama.



Katika makala hii tutajifunza jinsi Jinsi ya kufanya wateja wako kuipenda bidhaa/ huduma yako.





  • Huduma Kwa wateja - Kwa njia ya Sauti:


Hakikisha unatoa huduma kwa wateja kwa njia ya sauti hii ni kwea masaa 24 walau kwa siku 7 za juma. Itakufanya kujenga ukaribu na wateja wako na kuwafanya kuikumbuka bidhaa yako na mara kwa mara wanapokupigia simu na kutaka maelezo ya bidhaa yako hakikisha unatoa huduma iliyotukuka na kumpa mteja maelezo ya kumridhisha kuhusiana na bidhaa/ huduma yako.



  • Kuongeza Ubunifu


Unaweza kubuni kitu kitakachomfanya mteja kuipenda bidhaa yako , Mfano, Unaweza kumpa mteja wako warranty kwenye bidhaa yako hii itamfanya kuiamini na kuipenda bidhaa yako na Kuinunua. Unaweza kujiuliza ni kwa nini Samsung Bidhaa zao zinapendwa zaidi kwenye soko la Vifaa vya kielektroniki? Hii ni kwa sababu wanamuhakikishia mteja uimara na ubora kwenye bidhaa zao hii inaambatana na warranty.



  • Gharama Nafuu


Ushindani ni mkubwa, Unahitaji kufanya kazi kubwa na kuangalia njia za kuweza kupunguza gharama za uzalishaji viwandani na kutoa huduma bora kwa wateja wako bila gharama kuwa kubwa na kuwafanya kushindwa kununua.



  • Uzoefu wa kununua


Kuweka mijadala kwenye mitandao ya kijamii mfano Facebook,Jamii Forum, Instagram na hata vyombo vya habari ili kuwasiliana na wateja wako live na kuwapa wasaa wa kuuliza maswali, Kuweka sera rahisi za bidhaa yako, Masharti rahisi, Kuruhusu wateja kurudisha bidhaa kunapokuwa na kasoro ili kurahisisha uzoefu mnunuzi. Kufanya bidhaa yako kuwa rahisi kununua katika majukwaa yote, iwe unahifadhi offline au kwenye tovuti yako.



  • Kuelimisha wateja wako


Kama ndio unaanza kuuza bidhaa ambayo ndo mpya sokoni, hakikisha unawapa wateja wako elimu ya bidhaa yako kupitia mitandao ya kijamii , video, masoko na vyanzo vingine. Kuwaweka watu wanaohusika na mambo ya Kuitangaza na kuivutia bidhaa/ huduma yako. Kuandika hadithi zinazo walenga wateja wako na kuvuta wateja wapya.



  • Kuitangaza Bidhaa/ Huduma yako


Matangazo ya Bidhaa/ Huduma yako yatawafanya watu kujisikia Vizuri na kutambua kile wanacho kinunua toka kwako. Andaa kampeni kwenye mitandao ya kijamii, Matangazo ya barua pepe (Email marketing) Google adwords na kadhalika. Hii itawafanya wateja wako kuitambua na kuijua bidhaa yako.



  • Kuwa na uwazi


Kuwaonyesha wateja wako video za nyuma ya pazia kwenye uandaaji wa huduma/Bidhaa yako, Kuwatambulisha wafanya kazi wako na kuwaweka wazi kwa wateja hii itakusababisha kujenga Brand kubwa na kuwafanya wateja wako kuipenda bidhaa yako.



  • Rudisha sehemu yafaida kwa wateja wako.


Kuchangia mambo ya kijamii kwa kile unachopata kwa bidhaa/huduma yako. Wape offer wateja wako mfano; “nunua moja” “Pata moja bure!!” Hili ni wazo lililoanzishwa na Mjasiriamali mmoja aliyefahamika kwa jina la Tom Shoes, Lakini anaweza kutumia mfanyabiashara yeyote.

Kuanzisha bishara ni rahisi, Ila kuiendeleza na kwa mafanikio hii inahitajika jitihada za kila siku. Ifahamu nafasi yako sokoni na uongeze jitihada na kusonga mbele zaidi ya washindani wako na uongeze thamani ya huduma/ Bidhaa yako. Jaribu wateja wako muhimu na hakikisha unafanya tafiti za masoko na kuwafahamu washindani wako hii itakusaidia kujua mapungufu yao na mazuri yao na kukufanya kujiweka bora zaidi. Kama ukifuata ushauri huu nina uhakika utapiga hatua tano mbele zaidi ya hapo ulipo.


Hasante kwa muda Wako.


Makala hii imeandikwa na



Chrispin Kiure

Soft Clik(CF)

Website Design & Hosting | Graphics Design | Digital Marketing

info@softclik.com

+255 719786098
 
Back
Top Bottom