Braza Kede
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 3,840
- 6,844
Katika uzi huu tupia dondoo mbalimbali za kiusalama za kuzingatia katika mazingira ya nyumbani.
- Usilale na mitungi ya gesi ndani, tafuta sehemu nje ya nyumba uweke huko.
-Usiache nyaya za umeme zikiwa uchi, si salama.
- Weka vitu vyenye ncha kali kama visu, misumari, spoke, mbao au mabati yaliyotumika n.k kunakohusika, mfano kisu kikae jikoni, gereji au stoo.
- Hakikisha kuna mlango wa dharura unaokuwezesha kutoka kwenye matukio ya dharura kama moto, wizi nk.
- Hakikisha watoto wadogo (kama wapo) wanakuwa na uangalizi wa mtu mzima au mwenye uelewa kuweza kufuatilia nyendo zao na kuwaepusha na mienendo hatarishi.
- Hakikisha unakuwa na uelewa wa watu wanaofika hapo nyumbani kwako. Kumbuka kuwa mara nyingi wezi/majambazi wanakuwa sio watu wa mbali bali ni watu wanaopafahamu hapo kwako na aghalabu wanaweza kuwa wanashinda hapo kwako.
-Hakikisha unawafahamu wanaofanya kazi mbalimbali hapo kwako na kujiridhisha ninwatu safi. Hawa ni kama mafundi ujenzi, mafundi TV, mafundi wa matenki, mafundi bomba n.k.
- Kama kuna mashimo makubwa yaliyo wazi hakikisha yanazibwa ili watu wasitumbukie humo au kuwa mazalia au maficho ya wadudu hatarishi kama nyoka, mijusi n.k.
Tuendeleze kupeana tips wakuu....