TIRA yaja na stika za Bima za kielekroniki ili kudhibiti wizi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Kuanzia aprii 1, 2021 Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania(TIRA) imewatangazia wamiliki wa vyombo vya moto kuwa ulipiaji wa bima hautakuwa na utoaji wa stika za kubandika kama ilivyokuwa

Badala ya Stika za kubandika mteja atapewa namba ya kielekroniki ya stika. Hatua hii imefikiwa kutokana na kuendelea kwa uboreshaji wa mfumo wa kutunza kumbukumbu za bima za vyombo vya moto

Wameema wanafanya hivyo ili kupata huduma kwa haraka na kudhibiti upotevu wa mapato pamoja na uhalifu unaoweza kufanywa. Watoa huduma wa bima wametakiwa kuwaelimisha wateja wao

Mteja akikata bima atapewa Namba ya Stika ya kielekroniki, risiti ya malipo, hati ya bima na mkataba wa bima

1617380354753.png
 
Kwahiyo trafiki atakuuliza namba au?
 
Ngoja tuone.. Trafic anakwambia haya taja no yako ya bma chap....tukuchek😂😂😂😂😂
 
Kwahiyo trafiki atakuuliza namba au?
Bima ilishakuwa linked na systems za polisi , kila kimashine cha kuandika fine kina uwezo wa kupata taarifa za bima kwa chombo husika .
 
Nimekata juzi, nimepewa vyote walivyotaja isipokuwa hiyo namba ya kielektroniki
 
- Rudi ulipokatia bima wakupa ufafanuzi. Na pia wakuelekeze/wakuonyeshe kupitia mfumo ili usijesumburiwa na askari kuwa bima yako haipo kwenye mfumo wao/haujalipia.
 
Mi nasubiri tamko la kuwataka watoa bima KULIPA FIDIA YA AJALI NDANI YA LIMITED DAYS!
Siyo kila siku kukazana kubuni kukamata lakini wanaopata ajali wanatelekezwa
 
FB_IMG_16174354430883777.jpg

Kuanzia aprii 1, 2021 Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania(TIRA) imewatangazia wamiliki wa vyombo vya moto kuwa ulipiaji wa bima hautakuwa na utoaji wa stika za kubandika kama ilivyokuwa

Badala ya Stika za kubandika mteja atapewa namba ya kielekroniki ya stika. Hatua hii imefikiwa kutokana na kuendelea kwa uboreshaji wa mfumo wa kutunza kumbukumbu za bima za vyombo vya moto

Wameema wanafanya hivyo ili kupata huduma kwa haraka na kudhibiti upotevu wa mapato pamoja na uhalifu unaoweza kufanywa. Watoa huduma wa bima wametakiwa kuwaelimisha wateja wao

Mteja akikata bima atapewa Namba ya Stika ya kielekroniki, risiti ya malipo, hati ya bima na mkataba wa bima

View attachment 1741420
 
Khaaa...hahaha kudhibiti WIZI ? Humo humo ndani ujanja umekubuhu
FYI, wevi wana mbinu nyingi...
 
Back
Top Bottom