Wewe ndio naona umeanza siasa, hili la njaa huwa hatulifanyiia siasa au utani. Huwa tunakiri kila tukiwa na tishio na kulishughulikia.
Huko kwenu ndio naona mnatoa matamko tofauti kuhusu tishio la njaa.
Nilikua nafuatilia huu uzi hapa
Swali: Kuna Njaa au Hakuna Njaa Tanzania???.
Upande 01: Kuna Njaa Tanzania.
Upande 02: Hakuna Njaa Tanzania.
Serikali: Hakuna Njaa Tanzania.
Vyama vya Upinzani: Kuna Njaa Tanzania.
Viongozi wa Dini: Kuna Ukame na Njaa Tanzania, tumwombe Mwenyezi Mungu atuepushie mbali na hili.
Baadhi ya Wananchi: Kuna Njaa Tanzania.
Baadhi ya Wananchi: Hakuna Njaa Tanzania.
Wasomi na Wanataaluma kama Ma Dr na Prof. kwenye vyuo vyetu vikubwa wako kimyaaaa. Au wanatengeneza proposal wakafanye research kabisa kama kuna njaa Tanzania ama la!!!!.
Tunakumbuka sijui usemi usemao Mwenye shibe hamjui mwenye njaa????.
Kuna Njaa au Hakuna Njaa Tanzania???.