TISS Alhamis Mpaka Wikiendi

Mlenge

R I P
Joined
Oct 31, 2006
Posts
2,125
Reaction score
2,306
Tanzania Inter-bank Settlement System (TISS) πŸ˜‰ mwisho wa kazi siku ya Alhamis ni mchana saa sita mpaka Jumatatu asubuhi; kwa mujibu wa benki fulani.

Ukidipoziti cheki ya benki nyingine Alhamis mchana, watakuambia uhamishaji wa kupitia TISS utafanyika siku ya Jumatatu, na hivyo utegemee kuona salio likisoma siku ya Jumanne.

Yaani, siku zote hizo za kusubiri πŸ™

Pendekezo: TISS ifanye kazi saa 24, siku saba kwa wiki, wiki 52 kwa mwaka; 24/7/365.

Kwa mujibu wa kipeperushi cha TISS:

The TISS is an on-line system that facilitates real time and gross settlement of payment instructions between banks.

Online System kwa nini ifungwe masiku yote hayo? Suali kubwa la kujiuliza ni iwapo tunaweza kumudu gharama za kutofungua sistimu hiyo masaa yote siku zote; hata za sikukuu na wikiendi.

BTW, wabadilishe jina TISS kuwa linginewe, if they don't mind πŸ™‚.

EDIT: Disambiguation on the alleged timing of TISS services.
 
Mmmh!!Kwahiyo mfumo ndivyo ulivyowekwa siku hizi!!

Ngoja waje kukushambulia wanamfumo natoka kdogo
 
Nikweli kuna mambo yanazingua sana kwenye mfumo wetu wa kibenki mojawapo ni hili la TISS. Sijui kwann wana cutt-off time na jambo lenyewe ni online. Lkn kwenye swala la mwisho alhamis rudi kwenye hiyo benki ongea na mwingine yawezekana huyo mtu hajui, maana kuna benki nyingine nilishafanya weekend na mzigo ukaenda, pia muda wa saa sita pia sidhan km ni sahihi.
Jambo jingine ni hitaji la kutaka mtu unayemuwekea cheque asaini slip na cheque pia!! nmb walinikatalia mpaka jamaa asign na huku namlipa mtu yupo more than 450km away!! nikamuuliza je ingekua cash akasema hiyo haina shida, nikauliza je ingekua nalipa ada ya shule? akanyamaza nikasepa 😑😑
 

Muda wa saa sita ni kwa siku ya Alhamis. Nimeboresha maelezo. Maelekezo ya mwisho Alhamis nilipewa matawi mawili tofauti.
 
Mlenge, hao waliokueleza hivyo huenda ni wavivu tu wa kazi. TISS ipo mda wote wa saa za kazi, ni mfumo wa malipo unaohusika na kuhamisha pesa kutoka akaunti moja kwenda nyingine (funds transfer). Kwa sasa hivi kwa jinsi mifumo ilivyoboreshwa unaweza kuhamisha hela ndani ya nusu saa zikawa zimefika kwenye akaunti husika. Hundi (cheques) zina mfumo wake uitwao TACH (Tanzania Automated Clearing House). Kidogo nikijuacho ni hicho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaaah! Huu ujinga huu unanigarimu sana , nimeambulia patupu yaani.
 
Local Gment walizoea mwendo wa cheque na Epicor zao sasa hii TIS wanaona kama shetan kaja, mtanyoooka zama hizi.
 
Wanafanya hivyo maana wahuni wengi wanafanya kazi weekend
 
bbc , Kwa nini TISS iwe hewani saa za kazi tu? Kwa nini isiwe hewani mida yote? inawezekana isiyofanya kazi 24/7 ni hiyo TACH. Lakini wenye mabenki husema ni TISS ya kibenki mwisho Alhamis mchana.
 
bbc , Kwa nini TISS iwe hewani saa za kazi tu? Kwa nini isiwe hewani mida yote? inawezekana isiyofanya kazi 24/7 ni hiyo TACH. Lakini wenye mabenki husema ni TISS ya kibenki mwisho Alhamis mchana.
Nijuavyo mimi, "cut-off time" ya TISS ni saa 4 usiku kuanzia J3 mpaka J'mosi na mchana kwa siku ya J2. Huu ni mda ambao karibu taasisi zote (Benki kuu, benki za biashara na Serikali) zinakuwa zimemaliza kazi ya siku. Kumbuka hizo "transfers" zinafanywa na wafanyakazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…