PostGE2025 Tito Magoti: John Heche anashikiliwa na Polisi Osterbay anahojiwa kwa UGAIDI

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Bado tunaomboleza. Na tunatafuta miili ya ndugu zetu waliouwawa kwa risasi. Illegitimate President yuko ofisini siku ya pili. Hajajutia mauwaji aliyoyafanya. Wala kuomba msamaha. Au kuwafariji wafiwa na Taifa.

Ameona ampe kesi ya UGAIDI John Heche. Heche ameshikiliwa kwa siku 11 kwa tuhuma za uhamiaji—kwamba alivuka kwenda Kenya bila kufuata taratibu. Dola katili limeona limpe kesi ya Ugaidi. Yes, anahojiwa kwa ugaidi. Ukihusishwa na maandamano. Twende hivi hivi. Tutafika tu. Mungu.
​
 
Hahaha mbona kesi onaisha mapema hivi? Hamna namna wataweza ku tie hii kesi juu yake

Wanatafuta wa kumbebesha lawama but hawatofanikiwa
 
Inatia hasira sana
 
Msemaji mpya wa gesi la palisi au wa manerumango ama ni yule wakili?
 
Hahaha mbona kesi onaisha mapema hivi? Hamna namna wataweza ku tie hii kesi juu yake

Wanatafuta wa kumbebesha lawama but hawatofanikiwa
Itaisha pale watakapotaka, Mahakama ni za kwao
 
Ilitarajiwa, Lissu pia atapewa hiyo kesi ili akae ndani hadi 2030.
Wafuasi wa chadema wote watapewa kesi hizo hizo
Niffer naye atapewa kesi ya ugaidi
 
Taarifa ya Wakili Hekima Mwasipu[emoji1427]

“John Heche amepewa tuhuma za mbili:

1. Kujihusisha na vitendo vya kigaidi kutoka Kimara mpaka Magomeni; na

2. ⁠Kujihusisha na vitendo vya Kigaidi maeneo ya Msewe na Extenal.”

Hajatoa maelezo.

Yuko rumande.

Tumuombee.

Tumuunge mkono.
 
Taarifa kutoka Mkoa wa Kipolisi Kinondoni.
Makamu Mwenyekiti Mh. John Wegesa Heche amesafirishwa kutoka Dodoma leo hii na kuletwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni
Amepewa tuhuma za mbili:

1. Kujihusisha na Vitendo vya Kigaidi, kutoka Kimara mpaka Magomeni.

2. ⁠Kujihusisha na vitendo vya Kigaidi, maeneo ya Msewe na Extenal

Mara baada ya kutakiwa kuandika maelezo ya Onyo ametumia haki yake ya Kisheria ya kukataa kuandika maelezo na atatumia haki hiyo mara baada ya kupelekwa Mahakamani!. Taarifa zisizo rasmi muda wowote atapelekwa Mahakamani.

Hekima Mwasipu
Wakili
 
Tuna viongozi wendawazimu sana!
 
Watanzania wote tunatakiwa tuseme sasa basi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…