Tiwatope Savage Afunga Ndoa Siku Ya Jana Na Kupewa Gari

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Jana ilikua ni siku ya furaha kwa msanii “Tiwatope Savage” maarufu kama ‘Tiwa Savage’ ambae alifunga ndoa na mme wake “Tee Billz” ambae walikua wachumba kwa muda mrefu. Kabla hawajawa wachumba Tee alikua na meneja wa Tiwa msanii huyo kutoka nchini Nigeria. Ndoa yao imefanyika Dubai na ilihudhuliwa na watu maarufu peke yake.
Katika sherehe waliyofanya usiku wa jana msanii ‘Bank W’ aliwazawadia gari jipya wanandoa hao. Unaweza tazama picha za kilichojiri katika harusi hiyo.
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Gari Waliyopewa Kama Zawadi[/TD]
[/TR]
[/TABLE]






 
Napenda sauti yake...

Na Bank W ni nani kwao? mpaka awazawadie mkomko
 
Napenda sauti yake...

Na Bank W ni nani kwao? mpaka awazawadie mkomko

Bank W ni producer,pia uwa ana lebo yake na kuwa na wasanii ambao wako chini yake,pia yeye mwenyewe Bank W ni msanii wa RnB
 
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Millen na Tiwa Savage[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Miss Tanzania, 2001, Happiness Millen Magese, alihudhuria harusi ya kifahari ya mwanamuziki wa Nigeria, Tiwa Savage na Tunji Teebillz iliyofanyika kwenye hoteli ya Armani, iliyopo katika jingo refu zaidi duniani, Burj Khalifa mjini Dubai.
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Millen Magese na Don Jazzy[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Harusi hiyo ilifanyika Jumamosi, April 26.Miongoni mwa mambo yaliyotia fora kwenye harusi hiyo ni pale CEO MAVIN Records Don Jazzy alipowapa wanandoa hao gari mpya ya SUV.
Wageni wote kwenye harusi hiyo walipewa customized iPhones.
 
Uuuh haya bana wenye navyo wataongezewa....hongera zao
 
Millen Ana Mashosty Viwango Nollywood...

Halafu hata haringi, nilimuonaga kwenye msiba wa kanumba , she is soo cool, maana nilienda kuangalia tu umbea wa mastaa kila mtu alikuwa akiingia kwa mikogo as if walikuwa akina Beyonce au rihhana ila huyu demu kaingia xake kimya kimya bila hata ya mashauzi, nilichimpenda hakuwa mnafik kujifanya analia Lia ovyo maana wengine walikuw wanatak attention tu kwa kujifanya kulia sana
 

She Is A Lady Huyu My Binamu.....three Times A Lady....
 
Hawa ndo mastaa... Sio kila kitu ata ukienda kukojoa tu mbwembwe kibao kila mtu akujue.
 
nilimpenda sana siku hiyo..alikua na pilika full kuhudumia hapa na pale...
 
nilimpenda sana siku hiyo..alikua na pilika full kuhudumia hapa na pale...

Yah dah alikuwa anajituma kuliko hata bongo movie wenyew

Akina wema na wasanii wengine walikuwa wanajifanya wanazimia ovyo ili wasipembue michele na kuosha vyombo

Nilikuwa namchek mwanzo mwisho dah hana masihara kabisa wala hakutaka shobo na mtu
 
Yah dah alikuwa anajituma kuliko hata bongo movie wenyew

Akina wema na wasanii wengine walikuwa wanajifanya wanazimia ovyo ili wasipembue michele na kuosha vyombo

Nilikuwa namchek mwanzo mwisho dah hana masihara kabisa wala hakutaka shobo na mtu

Hahaaaa binamu mbavu zangu mie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…