tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kimesema kimejipanga kushiriki kikamilifu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, kwa kusimamisha wagombea katika kila jimbo, kata na uwakilishi Zanzibar, kikijinasibu kwa kaulimbiu yake ya “Kaza buti, barabara ina kokoto.”
Soma pia: CHADEMA na TLP zaungana na kukubaliana kuunda serikali ya Mseto, TLP itatoa Mwenyekiti na Chadema itatoa wale Wajumbe 5
Akizungumza leo, Ijumaa Agosti 29, 2025, jijini Dar es Salaam katika mapokezi ya mgombea Urais wa chama hicho, Katibu Mwenezi wa TLP, Bakari Makame amesema maandalizi ya chama hicho yanaonesha kuwa safari ya kuelekea kushika dola inawezekana.
“Sasa tunawaambia kweli kwamba tumejipanga. Tumeweka wagombea kila jimbo, kila kata na hata kwenye uwakilishi. Tunachofurahia zaidi ni kwamba idadi ya wagombea wanawake imekuwa kubwa kuliko wanaume, jambo linalotupa matumaini makubwa. Tunaamini kushika dola inawezekana,” amesema Makame.