Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Mgogoro wa kiuongozi ndani ya Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) umechukua sura mpya baada ya kundi la viongozi wa chama hicho, tarehe 29 Aprili 2025, kutoka mikoa mbalimbali nchini, kufika katika ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa jijini Dar es Salaam wakiwa na mabango, wakimlilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuingilia kati kutatua mvutano huo uliodumu kwa muda mrefu.
Viongozi hao wakiongozwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Bi. Dominata Rwechungura, walieleza kuwa wamelazimika kuchukua hatua hiyo baada ya kushindwa kupata majibu ya hoja zao kutoka kwa Msajili licha ya ahadi za mara kwa mara.
Mgogoro huo unadaiwa kuanza kufuatia mkutano mkuu wa chama uliofanyika tarehe 2 Februari 2025, ambapo wajumbe kutoka zaidi ya mikoa 20 walidai kutoshirikishwa na kutopata taarifa za mkutano huo. Katika mkutano huo, Bw. Richard Lyimo alijipitisha kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa, kinyume na hali ya awali ambapo wagombea walikuwa watano.
Hali hiyo ilizua sintofahamu kubwa ndani ya chama, hasa baada ya baadhi ya viongozi waliokuwa wakitarajiwa kugombea kujiengua au kuenguliwa katika mazingira yanayodaiwa kutokuwa ya haki. Viongozi hao wanaopinga mchakato huo wanasema kwamba hawapingi mtu binafsi bali wanapigania heshima ya Katiba ya chama na utaratibu wa kidemokrasia.
Wamesema kuwa wamejaribu kutafuta suluhu kupitia taasisi mbalimbali zikiwemo TLS (Chama cha Wanasheria Tanganyika) na Tume ya Haki za Binadamu, lakini bado hawajapata mwafaka wowote. “Tumechoka kusubiri majibu ya maneno matupu kutoka kwa Msajili. Tunamuomba kwa dhati Mheshimiwa Rais Samia aingilie kati atusaidie kumaliza mgogoro huu ili chama kiweze kufanya kazi zake kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi,” alisema mmoja wa viongozi hao.
Tangu kufariki kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa TLP, hayati Augustine Mrema mwaka 2022, chama hicho kimekuwa katika hali ya mashaka na mkanganyiko wa kiuongozi. Baada ya kifo chake, Eng. Aivan Maganza alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Taifa, lakini baadaye Bw. Richard Lyimo alijitokeza na kujitangaza kama Mwenyekiti mpya kupitia mchakato ambao baadhi ya wanachama wanaupinga vikali.
Source: Jambo TV