Uchaguzi 2020 TLP yatangaza kuungana na CCM. Yamteua Rais Magufuli kuwa mgombea Urais Oktoba 2020

Luqman mohamedy

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
899
Reaction score
1,231
TLP KUUNGANA NA CCM

Halmashauri Kuu ya Chama cha TLP imesisitiza kuwa chama hicho hakitasimamisha mgombea wa nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, badala yake chama hicho kitamuunga Mkono Mgombea wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli pindi atakapopitishwa na Chama Chake.

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho Augustino Lyatonga Mrema amesema maamuzi ya halmashauri kuu ya TLP yanafuatia chama hicho kuridhishwa na mwenendo wa utawala wa Serikali ya awamu ya Tano.

Your browser is not able to display this video.

















MAONI YANGU

Maamuzi ya TLP kumuunga mkono JPM kwenye uchaguzi wa 2020 inaweza kuwa na faida kubwa kwa TLP yenyewe kuliko hata CCM.

Sidhani na siamini kama CCM inahitaji kura chache za wanachama wa TLP, bali ninachodhani TLP wanahitaji nguvu na anagalau majimbo mawili matatu kwa nguvu ya CCM.

Hii ndio siasa bwana, ukikaza mashindano mwenzio anajenga muungano anakupiga bao.

Kama naona 2020 kwa mara nyingine TLP chama kilichokuwa mfu kinapata angalau kata na majimbo mawili.

Ukiona huna nguvu wewe ungana na mwenye nguvu baadae utapata nguvu.

UKAWA kuna tamaa kubwa muungano wao ni wa Kinafiki

Sina chama najaribu kuchambua muelekeo tu, usinicopy vibaya.
 
Nahitaji kadi ya TLP na katiba yao. Mwenye anaweza kunipa mwongozo anijulishe.
 
Mrema anajaribu kupanda mgongoni kwa CCM ili apenye uhakiki wa vyama utakaofanyika, mtihani mwingine kwa Chadema unakuja na jana msajili aliwachunia kwa makusudi kama ikulu.
 
Wamechagua fungu jema!
 
Hii ni vema ikaunganishwa na uzi mwingine nilioweka hapa kitambo .

Halafu utambue kwamba Magufuli si mgombea urais wa ccm , hajapitishwa na kikao chochote cha ccm , na kuna tetesi kwamba hatopitishwa na ccm
 
T
TLP kweli ina wanachama kweli? Chama maiti na mwenyekiti maiti!
 
Mzee wa parole anajua ana asilimia 0.00000000000001.
Ya kuchukua nchi.
ndo maana a anaona ili asipoteze muda bora ajiunge na ccm.
Na hivyo yupo parole

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani TLP ni chama cha siasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…