TheMaster
Member
- Aug 10, 2023
- 36
- 68
Habari wanajukwaa,
Binafsi nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa Raisi wa TLS na Mwanasheria mbobezi kwa jina maarufu la
Adv. Boniface Mwabukusi.
Kihistoria Mwambukusi inasemekana aliwahi kuwa mwanachama wa chama cha NCCR-Mageuzi lakini kwa kauli yake alikiri kuwa alijivua uanachama NCCR baada ya kuona mambo hayaeleweki kwa upande wake.
Jina la Mwabukusi liliibuka zaidi kipindi cha sakata la Mkataba wa Bandari na DP WORLD akijinasibu kuwa yeye ni Mwanaharakati na mtetezi wa Rasilimali za Tanganyika.
Huwenda kupaa kwa jina la Mwabukusi kipindi cha sakata la bandari ndio chachu ya Mwanasheria huyu kujikita zaidi kunako siasa na hata kijitweza katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya Urais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) na kushinda. Hongera kwake
Nikifatilia hotuba pamoja na kauli za kiongozi huyu mpya wa TLS napata wasiwasi kwamba huwenda TLS imebadilisha hadidu za rejea na kuwa ni chama cha siasa tena chenye lengo mama la kuiondosha CCM madarakani kupitia mgongo wa sheria.
Mwambukusi amekuwa akitoa kauli zenye kudhihirisha kejeli kwa serikali na CCM, dharau na hata vitisho kwa watawala na kuonesha kuwa TLS itasimama kidete ikiwezekana kutoa msaada wa kisheria kwa wote wanaohisi kuonewa na watala.
Soma Pia: Tushangilie ushindi wa TLS lakini tusitegemee mabadiliko TLS kupitia Mwambukusi; huyu ni mwanasystem kindakindaki
Mwabukusi alifikia hatua ya kutishia kuwa kama Rais wa TLS anaweza kuanzisha mgomo na maandamano endapo Serikali haitatii matakwa ya TLS.
Nadhani TLS ni jumuiya ya mawakili Tanzania na ni kama Jumuiya zingine mfano chama cha walimu Tanzania (CWT) au chama cha madaktari Tanzania (MAT) na wala sio Muhimili wa kuweza kuiwajibisha serikali au kushawishi wananchi kufanya chochote dhidi ya kitu chochote kwasababu TLS ina wajibu kwa mawakili ndani ya jumuiya yao na sio nje ya wanajumuiya wake.
Je, Mwabukusi anaeipeleka TLS kuwa chama cha Siasa?