TLS imefanya kazi nzuri sana. Kama hawataelewa hata uchambuzi huu, basi hawa itakuwa hawakuusaini na kuupitisha huu uchafu kwa bahati mbaya au kwa kukosa maarifa, bali walinuia kuliangamiza Taifa.
Na hapo itabidi tuchukue hatua dhidi ya hao waovu wanaotaka kuliangamiza Taifa.
Kama mwanasheria mkuu alishiriki kwenye mkataba huu, baada ya uchambuzi huu, ajiuzulu mara moja au afukuzwe haraka kwa namna yoyote inayotatikana.
Wale vidomodomo wasiojua chochote waje sasa, tuwasikie. Sijui kwa nini mara zote watu ambao huwa wanaipongeza na kuitetea serikali hata kwenye uovu, huwa ni wale ambao wana upeo na akili ndogo!!