Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 242
- 1,141
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kinalaani kitendo hiki kiovu na tunalitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua stahiki za kisheria na kuhakikisha wahalifu wote walio tenda kitendo kile na waliowezesha kutendwa kwa kitendo kile kiovu wanakamatwa na kufikishwa Mahakamani mara moja ili haki iweze kutendeka.
Aidha TLS inapinga vitendo vyote vya kikatili na udhalilishaji dhidi ya wanawake na iko tayari kushirikiana na vyombo vyote vya usalama na haki jinai katika kuhakikisha wahalifu hao wanafikishwa katika mamlaka sahihi za haki ili kujibu mashitaka yao. TLS pia kupitia kifungu cha 4 (e) cha Sheria iliyounda TLS (Tanganyika Law Society Act, Cap. 307 R.E. 2002) inaendelea kufuatilia mwenendo wa suala hili kwa ukaribu zaidi kwa kushirikiana na vyombo vya usalama na vinavyosimamia haki jinai ili kuhakikisha hatua stahiki kwa waliohusika zinachukuliwa kwa wakati na kwa mujibu wa Sheria.
Kila binadamu anastahili heshima, haki na usawa katika jamii yetu. TLS inatoa wito kwa jamii kusimama pamoja kupinga udhalilishaji, unyanyasaji na ukatili wa kijinsia wa aina yoyote ile ikiwemo kuacha mara moja kusambaza video zinazohusu tukio hili ili kulinda haki ya mhanga.
Tanzania bila udhalilishaji, unyanyasaji na ukatili wa kijinsia inawezekana!
Pia soma=> Polisi yaanza kufuatilia tukio la Binti aliyebakwa mande na wanaume watatu