Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 673
- 1,318
View: https://youtu.be/3DxH0NUxzRY?si=xZRKgw9HtibCALQv
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimeibua taharuki kubwa baada ya kupokea taarifa za kutishiwa maisha kwa mawakili watatu maarufu nchini Tanzania, Tito Magoti, Peter Madeleka, na Onesmo Ole Ngurumwa. Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na TLS tarehe 11 Septemba, 2024, chama hicho kimesema kimepokea malalamiko ya vitisho hivi moja kwa moja kutoka kwa wahusika.
TLS imeelezea vitendo hivi kuwa ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vinachukuliwa kwa uzito mkubwa kwani vinahatarisha uhuru wa kitaaluma na haki za binadamu nchini. Chama hicho kimesisitiza kuwa mawakili wana haki ya kisheria ya kutoa maoni na kuelimisha jamii kuhusu haki za raia na utawala wa sheria bila vikwazo vyovyote. TLS imeeleza kuwa vitisho vya aina hii sio tu vinaathiri utendaji wa mawakili bali ni vitisho kwa mhimili mzima wa mahakama nchini, wakiwemo waheshimiwa majaji na mahakimu.
Kwa hatua ya haraka, TLS imeitaka Serikali kupitia Jeshi la Polisi kuhakikisha usalama wa mawakili hao na kuchukua hatua kali dhidi ya wale wote wanaohusika na vitendo vya aina hii. Pia, chama hicho kimesisitiza umuhimu wa kufuata taratibu rasmi za kisheria katika kushughulikia tuhuma zozote zinazowahusu mawakili au raia wengine.
Hii si mara ya kwanza kwa mawakili na watetezi wa haki za binadamu kukumbana na vitisho vya aina hii. TLS imewataka wananchi na mawakili wote kutoa taarifa mara moja pindi wanapoona viashiria vya hatari kwa usalama wao.
Kwa kuzingatia mchango mkubwa wa mawakili katika kuhakikisha utawala wa sheria na utoaji wa haki nchini, hatua stahiki zinatarajiwa kuchukuliwa ili kulinda demokrasia na uhuru wa kisheria Tanzania.
11 SEPTEMBA, 2024.
TAARIFA KWA UMMA
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimepokea kwa masikitiko makubwa tarifa ya kutishiwa maisha mawakili Tito Magoti, Peter Madeleka pamoja na Onesmo Ole Ngurumwa. Tarifa hiyo tumeipokea kutoka kwa mawakili tajwa. TLS inalaani vitendo hivyo kwani ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
TLS, kwa mujibu wa kifungu cha 4(d) cha Sheria ya Chama cha wanasheria Tanganyika, inachukua kwa uzito usalama wa maisha ya wanachama wake wote. Aidha wakili ana haki ya kisheria ya kuzungumza na kutoa maoni yake bila vikwazo na ana haki ya uhuru wa kutumia haki hii katika kuelimisha jamii kuhusu Haki za Raia na Utawala wa sheria. Huu ndiyo Msingi Muhimu unao hakikisha uhuru wa Kitaaluma na Ulinzi wa Haki za binadamu, Utawala wa Sheria na Utawala bora. TLS inalaani vitendo vyovyote vinavyoashiria kutishia au kufifisha utendaji wa mawakili katika kazi zao kama Maofisa wa Mahakama na majukumu mengine waliyonayo kwa mujibu wa Kifungu cha 4 cha Sheria ya Mawakili Tanganyika. Vitisho vyovyote kwa wakili au mawakili ni vitisho kwa Muhimili wa MAHAKAMA, vitisho kwa Waheshimiwa Majaji na Mahakimu. Kwa ustawi wa Taifa letu, TLS inatoa wito kwa Serikali kutoruhusu hata kidogo kwa chombo hiki muhimu na kikubwa nchini chenye jukumu mahsusi la kutafsiri sheria na kutoa haki kwa watu wote, kutishiwa.
Mwisho, TLS inapenda kutoa wito kwa mamlaka za Serikali ikiwemo Jeshi la Polisi, lenye dhamana ya ulinzi wa raia na mali zake, kuhakikisha mawakili Tito Magoti, Peter Madeleka pamoja na Onesmo Ole Ngurumwa kama raia wengine wanakuwa salama wakati wote.
Endapo kutakuwa na tuhuma za kosa lolote lililofanywa na mawakili tajwa au mtu mwingine yeyote, vyombo husika vifuate taratibu rasmi za kisheria katika kushughulikia tuhuma hizo. Pia TLS inatoa wito kwa mawakili pamoja na wananchi ote kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola pindi wanapoona kunaviashiria vya kuhatarisha usalama wao.

Imetolewa na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)
Boniface A.K Mwabukusi
Rais
Boniface A.K Mwabukusi
Rais