TMA: Mvua hazitaendelea kunyesha, Wananchi wachukue tahadhari ya Hali ya ubaridi mkali

TMA: Mvua hazitaendelea kunyesha, Wananchi wachukue tahadhari ya Hali ya ubaridi mkali

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mifumo ya Hali ya Hewa haioneshi uwepo wa mvua hivi karibuni hapa nchini badala yake kutakuwa na ukavu na ubaridi ambapo Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari za kujilinda na baridi.

Meneja wa Utabiri wa TMA, Dkt. Mafuru Kantamla amesema mvua zilizonyesha hivi karibuni Ukanda wa Pwani zimetokana na ongezeko la Joto katika bahari ya Hindi hususani katika Mwambao wa Pwani lakini hazitakuwa na mwendelezo wa kwa kuwa joto la Bahari limeanza kupungua.

Chanzo: Torch Media
 
Back
Top Bottom