TMA ni Kama Taasisi Nyingi Za Serikali, Msishangae Kuambiwa Kuna Ukame

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Kama wengi mnavyofahamu, maeneo mengi mwaka huu yamekuwa na upungufu mkubwa wa mvua za vuli. Hata yale yaliyobahatika kupata, yamepata mvua kidogo sana kuliko ilivyo kawaida.

Hali hii inakuja kukiwa na matangazo mengi ya mara kwa mara ya TMA kuwa mwaka huu kutakuwa na mvua kubwa za EL nino, tena za kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa Duniani!! Tangazo lao la mwanzo ilitegemewa mvua hizo zianze mwezi September. Lakini mpaka sasa, meneo mengi yamekosa mvua hata zile za kawaida, achilia mbali hizo za El nino.

TATIZO LA TMA:
Kama zilivyo taasisi karibia zote zilizo chini ya Serikali kukosa umakini, na hii ni hivyo hivyo. TMA inakosa umakini katika utendaji wake. Sababu ya kusema kuwa kutakuwa na mvua za kutisha za Elnino, ni kuongezeka joto kwenye bahari. Kuongezeka kwa joto la bahari kunaweza kuongeza mvuke ambao hugeuka kuwa mawingu, na hatimaye mvua. Lakini hali hilyo ni uwezekano, siyo LAZIMA.

TMA wamekuwa wakitangaza uwezekano, kama jambo la LAZIMA. Haya ni mapungufu makubwa kwa wataalamu wa TMA. Utabiri hata siku moja hauwezi kuwa uhalisia kwa 100%, lakini kwa kukosa umakini, TMA wamekuwa wakitangaza kuwa mvua za El nino, lazima zitatokea, badala ya kueleza kuwa kuna uwezekano, lakini siyo lazima itokee, wo wanasema lazima kutakuwa na mvua za El Nino, ilihali hawana utaalam bali wanategemea zaidi matamko ya taasisi za mbali ambazo siyo lazima zizingatie hali halisia za eneo husika.

Taasisi mbalimbali za kisayansi Tanzania hazifanyi tafiti zozote za kitaalam, na hivyo kubakia kuwa messengers wa taasisi za nje. Kiuhalisia, kuongezeka kwa joto la bahari siyo sababu pekee ya kupata mvua kubwa.

Kiuhalisia, kwa hali ilivyo mpaka sasa ya kukosa hata zile mvua za kawaida za vuli, wala msishange kushuhudia upungufu wa mvua kwa maeneo mengi. Taarifa za TMA siyo uhakikisho, bali ni utabiri ambao uaweza kutokea au hata kuwa kinyume chake.

About natural occuring phenomena, no one is confident 100%. That is the reason for such events causing unexpected calamities, because in most cases they hapoen at unexpected time. Good to take precautions based on prediction but no one should fool people that it must happen because of ocean temperature surge.

Tumshukuru Mungu wetu, balaa lililipigiwa sana na watu, mpaka sasa halipo. Mungu anazidi kudhihirisha ukuu wake.
 
Watu wamesafisha mifereji, kujenda Kingo za kuelekezea maji, kumbe elnino ni haki ya joto Kali?

TMA wamenizingua

Mbaya zaidi tumekata miti yetu ya vivuli na Sasa jua Kali
 
TMA ni jumuiya ya chama cha Mbumbumbu
 
Watu wamesafisha mifereji, kujenda Kingo za kuelekezea maji, kumbe elnino ni haki ya joto Kali?

TMA wamenizinguq
Joto kali husababisha mvuke mwingi kwenda angani,kwa jiografia ya darasa la tano,huo mvuke baadae huwa mvua,so ukiwa mwingi na mvua huwa nyingi,zingatieni elimu
 
Mm na rejea World Meteorogical Organization (WMO), na wamesema kutakua na mvua kubwa kati ya Oct - February.

Na tukumbushane tu, mvua kubwa zitakuepo zikifuata vipindi vya siku zote vya mvua.

kama uliko zinaanzaga mwezi wa 11 basi subiri mwez wa 11 zianze
 
Back
Top Bottom