TMA: Viwango vya Joto Njombe, Iringa na Mbeya kufikia 4°C

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imesema kwamba hali ya baridi itaendelea kuwepo ambapo katika mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya baridi inatarajiwa kufikia viwango vya chini vya nyuzi joto 4°C.

ukunguuu.jpg
Ukungu wa baridi
Akizungumza hii leo jijini Dar es Salaam, Mtaalam wa uchambuzi wa hali ya hewa kutoka TMA Rose Senyagwa, amesema hali ya mvua zinazonyesha ni za nje ya msimu ambapo zimetokana na hewa kunyonya unyevunyevu baharini na hivyo kupelekea mvua hizo kunyesha.

Kuhusu hali ya barafu iliyojitokeza hivi karibuni mkoani Njombe, Senyagwa amesema hali hiyo inayofahamaika kama Sikitu inatokana na majimaji ya unyevunyevu kuganda na hivyo kupelekea barafu hizo hali ambayo ni kawaida kunapokuwepo na baridi kalI

Chanzo: EATV
 
Miaka minne iliyopita nilikuwa na ziara Makete mwezi wa sita na wa saba, hakika kule sio sehemu ya kuishi kabisa. Unafikia Kitulo (wanaita Bustani ya Mungu) hapo ni balaa kwa baridi. Kule wanakuweza wenyewe na kwa sasa kila ikitokea nafasi ya kwenda kule, naipiga chenga
 
Sio mchezo
 
Shida ni kiswahili.
Temperature = Joto. I feel hot = Nasikia joto. Hot (heat) ni tofauti na temperature maana temperature ni kipimo cha umoto moto (hot) au ubaridi (cold). Kwa hiyo tatizo ni kwa temperature na hot kuwa na tafsiri sawa wakati mwingine wakati ni maneno mawili yenye maana tofauti.

ILA SITOKEI TMA.
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imesema kwamba hali ya baridi itaendelea kuwepo ambapo katika mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya baridi inatarajiwa kufikia viwango vya chini vya nyuzi joto 4°C.

ukunguuu.jpg

Akizungumza hii leo jijini Dar es Salaam, Mtaalam wa uchambuzi wa hali ya hewa kutoka TMA Rose Senyagwa, amesema hali ya mvua zinazonyesha ni za nje ya msimu ambapo zimetokana na hewa kunyonya unyevunyevu baharini na hivyo kupelekea mvua hizo kunyesha.

Kuhusu hali ya barafu iliyojitokeza hivi karibuni mkoani Njombe, Senyagwa amesema hali hiyo inayofahamaika kama Sikitu inatokana na majimaji ya unyevunyevu kuganda na hivyo kupelekea barafu hizo hali ambayo ni kawaida kunapokuwepo na baridi kalI

Chanzo: EATV
Sawa, kitakuwa kama Ulaya. Si huwa unaona kwenye mechi huwa kuna vibarafu vinaanguka.
 
Miaka minne iliyopita nilikuwa na ziara Makete mwezi wa sita na wa saba, hakika kule sio sehemu ya kuishi kabisa. Unafikia Kitulo (wanaita Bustani ya Mungu) hapo ni balaa kwa baridi. Kule wanakuweza wenyewe na kwa sasa kila ikitokea nafasi ya kwenda kule, naipiga chenga
Unawambiaje watu wa Greenland na Siberia ambako barafu iko full time

Sema sio sehemu ya kuishi wewe
Mimi nimeishi makete ile hali ya hewa kunastawi sana mazao ya ngano,pareto na viazi mviringo .Kuna uzalishaji mkubwa hasa sio utani

Na watu wanaishi kule kuko poa tu mbona

Una roho ya kimaskini sio ya kutafuta utajiri
 
Back
Top Bottom