TMA: Viwango vya Joto Njombe, Iringa na Mbeya kufikia 4°C

Nadhani kaizungumzia kama utani tu..
 
Umasikini unao wewe, mimi sina dhiki hiyo
 
Hii Hali Kwa wakulima wanaenda mashambani kweli? Sidhani kama unaweza kupata nguvu ya kulima tena Kwa jembe la mkono
Mkuu nimekaa Njombe kwa muda fulani..yaani wenyeji shuguli wanafanya kama kawaida ni kama hakijatokea kitu hata wewe mgeni ukishazoea unaona kawaida...ukizoea kuna muda hasa mchana unaweza tembea bila sweta.

Mimi nilikua naoga maji ya baridi kama yalivyo nilivyozoea na ilikua safi safi tu.
 
Kweli kabisa mkuu. Makete pazuri sana hususan kuanzia pale Ikonda, Kisinga, Iwawa, Bulangwa na Iniho. Ukishazoea kuishi kule hutotaka tena kuondoka manake kila aina ya matunda (temperate fruits)na mazao ya chakula unapata bila kusahau kinywaji pendwa cha Ulanzi. Maji yote ni maji baridi hakuna maji ya chumvi na ukitaka eneo lenye joto nenda Matamba karibu na Chimala.
 
Tutarajie mazao kuungua sana hasa viazi chipsi na nyanya
Hiyo kweli ndo itakuwa changamoto. Wakulima wajitahidi kuzingatia maelekezo ya Wataalam ni nini cha kufanya ili walau kupunguza athari zitokanazo na barafu hiyo.
 
Hiyo Hali ipo Tangu Juzi wao walikuwa kimya tu Hawa TMA wanachelewa sana kuhabarisha wananchi walitakiwa wawe wanatoa angalizo/taarifa masaa 24/48 kabla
 
Tutarajie mazao kuungua sana hasa viazi chipsi na nyanya
Chips na nyanya zinaungua njombe
Sio makete. Makete viazi chips vinalimwa miaka na Miaka hakuna shida na kuna baridi kali.

Njombe ndio wana experience baridi kali huwa haiko kali sana kama ya mwaka huu

Makete ni normal. Baridi Kule kali sana kawaida haijaanza leo

Milima ni vipara Haina miti ya asili shauri ya baridi. Kule hukuti mbu
 
Wewe mkuu umechemka matamba kuna joto, matamba ndio Kituro, huku ndio kilele cha bardi tz
 
Hatari sana mkuu nahisi Mimi kama naingia Njombe Leo nitaishia kukaa ndani tu
 
Umasikini unao wewe, mi sina dhiki hiyo
Mtu yeyote anayeangalia hali ya hewa kwenyeb sehemu ambako kuna utajiri halafu anasema sio pa kuishi ana pepo au shetani la umaskini. Wewe ni mmojawapo.Nenda kaombewe
 
Wewe mkuu umechemka matamba kuna joto, matamba ndio Kituro, huku ndio kilele Cha bardi tz
Matamba ni Kituro? Nazungumzia Matamba pale penye mji na viunga vyake kabla hujazianza zile kona 54 kuelekea Chimala. Labda Matamba kama Tarafa nakubali. Lakini Kitulo ni Mlimani kule lilipo shamba la mifugo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…