TMA yatabiri joto kali na ukame

Mamlaka ya hali ya hewa imetoa utabiri wake kama unavyoonekana hapo[emoji116] ila huko mbeleni naona dhahama kubwa kwa sisi wakulima inakuja!
 
Ukiona MTU ana beza taarifa za kitaalamu kama hizo jibu ni simple tuuu " shule hana"
Nimekuwa nikifuatilia hizi taarifa za utabiri kwa miaka kadhaa ukweli zimenisaidia sana kujipanga na zina usahihi mkubwa, mwaka jana zimeniepusha na hasara kubwa shambani iwapo ningepanda mapema.

Tma wanatakiwa watoe detailed report kwa kila specific area wilaya/kata. SI sahihi kusema mbeya/…njombe itakuwa hivi hali ya hewa na mvua ya chunya, mbarali, kyela na rungwe ni tofauti. Generalization ni tatizo kwenye hii mamlaka.

Mfano ndani ya wilaya moja kuna kata zinapata mvua kuanzia October nyingine mvua ya kwanza December, mtaa huu mvua inapiga 24 hrs mtaa mwingine pakavu
 
Mwambie huyo Hamza sisi wenyewe tumeshaona hali ya hewa ilivyo.
Hakuna haja ya utabiri,yeye aendelee kukaa ofisini mshahara ataendelea kupokea.
 
Geita tunalimaga mwezi wa 9 au wa 10.
Sa sijui hapa vp
 
Hizi habari huwa hazituhusu sisi wa Nyanda za Juu Kusini ,sijawahi shuhudia ukame landa mvua kuzidi ila mikoa ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa daa nimeshuhudia mara kadhaa ila msijali kufa kufaana tutawalisha ila kwa bei juu.

Ule msimu wa kuuza dume kubwa la ng'ombe kwa gunia umefika.
 
Huku kanda ya ziwa kina cha ziwa Victoria kwa kipindi cha miezi michache tu naona maji yanapungua kwa kasi sana,

Mungu tuepushie mbali na hili balaa.
 
Na hii hali itakuwa ngumu sana kwa huu uchumi wa tozo hasa endapo kutakuwa na upungufu mkubwa wa uzalishaji chakula na pia kupungua kwa vyanzo vya maji.....
 
TMA wameshaweka mkeka tayari wanasubiri tu bet won au bet lost
 
Pwani ya kaskazini, kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, mikoa ya Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia, Dar es Salaam na Tanga, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Panahitajika ufafanuzi binafsi sijapaelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…