Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la mvua kubwa katika mikoa minane kuanzia leo Jumanne, Desemba 3, 2024.
Mvua hizo katika mikoa hiyo ya Dodoma, Singida, Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa, Songwe na Manyara.
Taarifa hiyo ya TMA iliyotolewa leo Desemba 3, 2024 imetahadharisha wakazi wa mikoa hiyo kuchukua tahadhari kutokana na wingi wa mvua hizo.
"Desemba 4, 2024 angalizo la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya nyanda za juu kusini magharibi mikoa ya Iringa, Njombe, Rukwa na Songwe.
"Kanda ya kati Dodoma na Singida na Mkoa wa Morogoro, athari zinazoweza kujitokeza ni makazi kuzungukwa na maji," inasema TMA.