TMA yathibitisha El Nino, mvua za awali zimeanza

TMA yathibitisha El Nino, mvua za awali zimeanza

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema hali ya El Nino nchini inaendelea kuimarika, huku kilele chake kikitarajiwa kufikiwa katika kipindi cha Novemba na Desemba.

Ofisa Habari wa TMA, Ramadhan Omary katika taarifa yake Jumapili, Septemba 27, 2026, kwamba El Niño tayari imejijenga na kinachoendelea sasa ni kuimarika kwa hali hiyo, huku mifumo ya hali ya hewa ikionyesha nguvu yake itaongezeka kadiri mwaka unavyoelekea mwishoni.

"Uwezekano wa kuwepo El Nino ni asilimia 100, kwa maana tayari imeshajitengeneza. Kinachoendelea kwa sasa ni kuimarika kwa kwa hiyo hali,"

Kwa mujibu wa Omary, mvua zimeanza kujitokeza katika baadhi ya maeneo kabla ya msimu kuimarika, huku maeneo yanayozunguka Ziwa Victoria yakitarajiwa kupata mvua kuanzia mwishoni mwa Septemba hadi wiki ya kwanza ya Oktoba.

Alisema mikoa ya Kagera na Mara ni miongoni mwa maeneo ambayo tayari imeanza kupata mvua za hapa na pale pamoja na ngurumo.

"Zipo ripoti katika mfumo kwamba kuna mvua za hapa na pale, pia kuna ngurumo, hususan katika maeneo ambayo yanazunguka Ziwa Victoria, kwa maana ya mikoa ya Kagera pamoja na Mara,"
IMG-20260928-WA0005.jpg
 
Kweli mvua zimezidi wastani .Kuna mvua imenyesha huku nilipo ni hatari
 
Huku kwetu nahsi inaweza isifike maana ni kukavu,jua ni kali na hakuna hata dalili hata ya manyunyu...
 
Joto limeongezeka inaonekana mvua zitanyesha za maana, sio utani.
 
Back
Top Bottom