Wakuu,
View attachment 3264417
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa utabiri wa mvua kubwa katika Mikoa ya Kigoma, Katavi, Tabora, Singida, Dodoma, Simiyu, Mara, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Kagera, Geita, Mwanza na Shinyanga, Tanga, Morogoro, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Mtwara, Lindi, Rukwa, Mbeya, Iringa, Songwe, Njombe na Ruvuma pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Aidha Kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni wastani, baadhi ya makazi kuzungukwa na maji.
Utabiri huo umetolewa Machi 8, 2025.