TMA yatoa utabiri wa mvua kubwa katika mikoa 25

Na iwe hivyo maana si kwa joto hili!
 
Huu ni uongo kwa kanda ya kati, msimu wa mvua umeisha. Ila kwa pwani msimu ndo unaanza inaweza ikawa kweli.
 
Huku Kagera imeanza jana

Ila ya leo ilikuwa kubwa mnooo mixer upepo
 
Wiki iliyopita ilinyesha hiyo mvua ase nibalaa, baadhi ya ziliezuka na nguzo zaumeme kuanguka
 
Jana walitabiri na kweli ilinyesha kiasi chake katika mkoa mmoja wapo hapo
 
Angalau si kwa joto hili, ilikua imeanza kupelekea mazao kuchangamka bei
 
Wacha inyeshe maana huku kwetu kinolewo jua limewaka kweli mweli mpka pumbuz zinatoka jasho bwana
 
Sasa husemi ni lini hiyo mvua itanyesha, ni utabiri huo?
Kwa kawaida wao huanza na sentensi hii, "utabiri wa hali ya hewa katika kipindi cha masaa 24 ijayo" . Yaani kuanzia wakati huo hadi 24 hours later. Hii hutolewa kwenye vipindi vya kila siku vya radio na televisheni, nk.

Na kuna wakati wanatoa extended weather forecast kwenye website yao na kama taarifa maalum I think kwa vyombo vya habari kwa ujumla. Mfano mwezi Januari or early Februari walitoa utabiri kuwa kutakuwa na uhaba wa mvua maeneo mengi ya nchi hadi mwezi March 2025 , na walisema joto litakuwa kubwa juu ya wastani. Na ndivyo ilivyokuwa. Nadhani tuna kawaida ya kusahau tu. Na walitoa hiyo taarifa wakati maeneo mengi mvua zilikuwa bado zinanyesha sana.

Hata hivyo, utabiri si kila kitu lazima kiwe 100% kila mahali. Mfano huenda mvua zikanyesha mikoa hiyo yote, lakini si lazima kila kijiji, kija mji au wilaya zipate hizo mvua.
 
Ni almost Tanganyika Jana kibaha ilipiga jaramba
 
Wamepatia, niko kanda ya kati muda huu mvua ya kutosha kudondosha maji mengi inanyesha. Ila mazao kama mahindi yaliishakauka hasa ardhi ya kichanga na miinuko, ardhi ya mbuga yalivumilia ukame mpaka mvua ikarudi. Uwele haukuathirika kwa ukame uliotokea wa mwezi mmoja.Pamoja na kurudi kwa mvua machi hii imebaki mwezi mmoja tu wa aprili msimu wa mvua kanda ya kati umalizike na wakulima watatumia mvua za mwishomwisho kupanda alizeti na dengu kwa ukanda wa kati wenye msimu mmoja tu wa mvua kwa mwaka. Kutokana na kukatika kwa mvua mwezi februari/machi mwaka huu kutakuwa na upungufu wa mavuno ukanda wa kati wenye kutegemea msimu mmoja wa mvua
 
Hata hizo probability nazo si zina siku za kutokea!! Nacho maanisha waseme kwamba kuanzia wiki au mwezi na mwaka fulani mvua itaanza kunyesha!!
Sasa kutajiwa mikoa 15 mvua itanyesha ni mwezi ujao au mwaka 2027??
Akisema siku na isitokee hutawaamini.
Our mind nature is against probabilistic thinking.
They can't comprehend with probability
 
Ni kweli huku niliko imenyesha mvua kubwa leo 9/03!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…