Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba Nchini (TMDA), Bw. Adam Fimbo ametoa rai kwa jamii kutambua dawa zote za antibiotiki (Antibiotic) endapo watazitumia kwamba ni lazima iwe na matokeo ikiwemo harufu katika mkojo wa mtumiaji baada ya kutumia.
“Kama hutasikia harufu katika dawa hiyo ujue hakuna dawa humo, kinyesi kisipokuwa cheusi ujue hamna dawa humo ndani ya hiyo dawa. Kila dawa inamatokeo yake baada ya kutumia lakini isipotoa matokeo husika ujue dawa hiyo ni bandia hivyo inatakiwa hatua kuchukuliwa haraka,” Alisema Fimbo
Pia Fimbo ameitaka Jamii kuwa watambuzi kwenye kuzingatia dawa halisi ama bandia huku akisema kuwa dawa zote zilizosajiliwa nakukaguliwa na TMDA zinatakiwa kuwa na namba za TMDA za usajili ili kuwahakikishia watumiaji ubora na viwango vilivyokusudiwa katika matumizi.
“Dawa zilizosajiliwa na TMDA zina nembo inayoanzia na TZ na nembo ya dawa inayoanzia na TZA ambapo kila unapoangalia lebo ya dawa utaona namba hizo ambazo zitakuhakikishia kwamba dawa hiyo imesajiliwa na TMDA,” Alisema Fimbo
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TMDA, anayeshughulikia dawa na vifaa tiba Dkt. Yonah Mwalwisi amesema mamlaka hiyo inatumia mbinu na mifumo mbali mbali inayosaidia kudhibiti ubora katika soko la nchi kwa kuhakikisha linapata vitendanishi na vifaa vyenye ubora, salama na vyenye ufanisi unaotakiwa.
EATV
Bw. Fimbo ametoa rai hiyo wakati wa akifungua rasmi mafunzo ya siku nne kwa wakaguzi wapya yanayofanyika Kibaha, Mkoani Pwani ambapo alibainisha kuwa TMDA, ina utaratibu wa mafunzo hayo ya mara kwa mara kwa ajili ya kuwajengea uwezo wakaguzi ilikuzuia mianya ya kuingiza dawa bandia ama zisizo na ubora kwa matumizi ya binadamu.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba Nchini (TMDA), Bw. Adam Fimbo