TMDA: Ukitumia antibiotiki na usipokojoa mkojo wenye harufu, jua hiyo ni bandia

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba Nchini (TMDA), Bw. Adam Fimbo ametoa rai kwa jamii kutambua dawa zote za antibiotiki (Antibiotic) endapo watazitumia kwamba ni lazima iwe na matokeo ikiwemo harufu katika mkojo wa mtumiaji baada ya kutumia.

tmmma.jpg

Bw. Fimbo ametoa rai hiyo wakati wa akifungua rasmi mafunzo ya siku nne kwa wakaguzi wapya yanayofanyika Kibaha, Mkoani Pwani ambapo alibainisha kuwa TMDA, ina utaratibu wa mafunzo hayo ya mara kwa mara kwa ajili ya kuwajengea uwezo wakaguzi ilikuzuia mianya ya kuingiza dawa bandia ama zisizo na ubora kwa matumizi ya binadamu.

“Kama hutasikia harufu katika dawa hiyo ujue hakuna dawa humo, kinyesi kisipokuwa cheusi ujue hamna dawa humo ndani ya hiyo dawa. Kila dawa inamatokeo yake baada ya kutumia lakini isipotoa matokeo husika ujue dawa hiyo ni bandia hivyo inatakiwa hatua kuchukuliwa haraka,” Alisema Fimbo

Pia Fimbo ameitaka Jamii kuwa watambuzi kwenye kuzingatia dawa halisi ama bandia huku akisema kuwa dawa zote zilizosajiliwa nakukaguliwa na TMDA zinatakiwa kuwa na namba za TMDA za usajili ili kuwahakikishia watumiaji ubora na viwango vilivyokusudiwa katika matumizi.

“Dawa zilizosajiliwa na TMDA zina nembo inayoanzia na TZ na nembo ya dawa inayoanzia na TZA ambapo kila unapoangalia lebo ya dawa utaona namba hizo ambazo zitakuhakikishia kwamba dawa hiyo imesajiliwa na TMDA,” Alisema Fimbo

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TMDA, anayeshughulikia dawa na vifaa tiba Dkt. Yonah Mwalwisi amesema mamlaka hiyo inatumia mbinu na mifumo mbali mbali inayosaidia kudhibiti ubora katika soko la nchi kwa kuhakikisha linapata vitendanishi na vifaa vyenye ubora, salama na vyenye ufanisi unaotakiwa.

EATV
Kwahiyo sisi wananchi ili tugundue kama ni feki. Inabidi tuitumie kwanza?? Sasa kama ni madhara yatanikuta kwanza?
 
wasomi wetu bwana .. mama akiwagusa mnahisi kuonewa why mpaka ifike tumboni mtu akojoe ingieni huko zinako uzwa mkazipime kabla ya wananchi kuzitumia mianya ya fake mnaijua sana aah tusije laumu mamlaka ukiguswa.
 
Mimi nimekuelewa vizuri sana.

Asante kwa kutustua.

Lakini imarisheni mifumo ya kuzuia fake zisiingie nchini.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba Nchini (TMDA), Bw. Adam Fimbo ametoa rai kwa jamii kutambua dawa zote za antibiotiki (Antibiotic) endapo watazitumia kwamba ni lazima iwe na matokeo ikiwemo harufu katika mkojo wa mtumiaji baada ya kutumia.

tmmma.jpg

Bw. Fimbo ametoa rai hiyo wakati wa akifungua rasmi mafunzo ya siku nne kwa wakaguzi wapya yanayofanyika Kibaha, Mkoani Pwani ambapo alibainisha kuwa TMDA, ina utaratibu wa mafunzo hayo ya mara kwa mara kwa ajili ya kuwajengea uwezo wakaguzi ilikuzuia mianya ya kuingiza dawa bandia ama zisizo na ubora kwa matumizi ya binadamu.

“Kama hutasikia harufu katika dawa hiyo ujue hakuna dawa humo, kinyesi kisipokuwa cheusi ujue hamna dawa humo ndani ya hiyo dawa. Kila dawa inamatokeo yake baada ya kutumia lakini isipotoa matokeo husika ujue dawa hiyo ni bandia hivyo inatakiwa hatua kuchukuliwa haraka,” Alisema Fimbo

Pia Fimbo ameitaka Jamii kuwa watambuzi kwenye kuzingatia dawa halisi ama bandia huku akisema kuwa dawa zote zilizosajiliwa nakukaguliwa na TMDA zinatakiwa kuwa na namba za TMDA za usajili ili kuwahakikishia watumiaji ubora na viwango vilivyokusudiwa katika matumizi.

“Dawa zilizosajiliwa na TMDA zina nembo inayoanzia na TZ na nembo ya dawa inayoanzia na TZA ambapo kila unapoangalia lebo ya dawa utaona namba hizo ambazo zitakuhakikishia kwamba dawa hiyo imesajiliwa na TMDA,” Alisema Fimbo

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TMDA, anayeshughulikia dawa na vifaa tiba Dkt. Yonah Mwalwisi amesema mamlaka hiyo inatumia mbinu na mifumo mbali mbali inayosaidia kudhibiti ubora katika soko la nchi kwa kuhakikisha linapata vitendanishi na vifaa vyenye ubora, salama na vyenye ufanisi unaotakiwa.

EATV
Heee hana hata PhD inamana
 
Bongo bhana, unashauriwa u test sumu kwa kuimeza, tena na namlaka husika kabisa.
 
Sio lazima ukojoe, hata ukiibomoa moja ukailamba utajua kama ni fake au?
 
Kwahiyo verification ya dawa ni mkojo na choo? Wadhibiti dawa bandia kabla hazijatufikia kuliko kutufanya miili yetu sehemu za majaribio
 
Yani imagine mtu unaumwa umeandikiwa dawa na kuanza kutumia lakini huponi maumivu yanazidi kumbe sababu dawa fake [emoji15][emoji15]

Jamani Mbona mtihani mkubwa huo.

Zuieni zisiingie nchini bana.
 
Wewe na mkurugenzi akili zenu ni sawa.....[emoji23][emoji23][emoji23] Hivi dawa zote tunazotumia end product inatolewa na figo?

Ifike pahala, tuache wataalamu waongee na tuache siasa kwenye taaluma nyeti
 
Hata hivyo katika kunywa dawa kwangu kote dawa ambazo zimekuwa zikitoa harufu kwenye mkojo ni zile zenye kiambata cha Amoxicillin na jamaa zake. Hizo nyingine harufu huwa naihisi mdomoni tu.
 
Back
Top Bottom