Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ila kwenda chooni ni kwa vile ni lazima hakuna muhali. Ila kwenda huko na kuvuta sigara kwenye ile harufu naisubiri hadi nifikapo nyumbani ambako mwenye mamlaka ya mwisho ni mimi mwenyewe.Vutia chooni bwashee
Hujakatazwa kuvuta ila vuta kistaarabu. Kuna watu sio wastaarabu na masigara yao wanavuta pasipo kuangalia wapo maeneo ganiKama ndio hivyo kwa nini wasipige marufuku kilimo cha tumbaku.
wavutie wapi sasaMamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imesema ni kosa kisheria kuvuta sigara hadharani au kwenye maeneo ya mikusanyiko na atakayebainika kufanya hivyo atatozwa faini ya Tsh. 200,000 au kutumikia adhabu ya kifungo cha miezi sita jela.
Meneja wa Kanda ya Mashariki wa TMDA, Gloria Matemu aliyasema hayo Aprili 9, 2022 katika Soko Kuu la Kariakoo, wakati wa kampeni ya kutoa elimu katika maeneo ya mikusanyo kuhusu madhara ya kutumia tumbaku na adhabu zake.
Alisema TMDA imepewa jukumu la kudhibiti matumizi ya tumbaku kwa lengo la kutoa elimu kuhusu matakwa ya sheria namba 121 kuanzia Aprili 30, 2022.
"Ukibainika unavuta tumbaku hadharani au katika mikusanyiko utatozwa faini ya Sh 200,000 au kutumikia adhabu ya miezi sita jela," alisema.
Hivyo, aliwataka wamiliki wa kumbi za starehe na masoko kutenga maeneo maalum ya kuvutia sigara kwa sababu watu wengi wanaathirika kutokana na watu wachache wanaovuta sigara.
Matemu alisema TMDA imefanya kampeni ya siku tano ya kutembelea kwenye maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu kama vituo vya mabasi na masoko, ili kuwaelimisha kuhusu madhara na namna sheria inavyofanya kazi.
Alisema kampeni hiyo imesaidia kufikisha elimu kwa wakazi wa Manispaa ya llala na lengo kuu ni kuwafikia Watanzania wote wafahamu kuhusu jukumu hilo la TMDA katika kudhibiti matumizi ya tumbaku ili kupunguza madhara yatokanayo na uvutaji huo.
Mkaguzi wa TMDA, Kanda ya Mashariki, Jafari Tolo alisema takwa la sheria ni kuzuia uvutaji wa sigara kwenye mikusanyiko ya watu na wamiliki wa maeneo yanayokusanya maeneo maalum ya wanaovuta kuvuta bila kuathiri wasiovuta.
Alisema pia maeneo yenye mikusanyiko kunapaswa kufungwa vifaa vya kubaini endapo kuna mtu anavuta sigara katika maeneo yasiyoruhusiwa.
Ofisa Afya wa Soko la Kisutu, Aron Matei aliishukuru TMDA kwa elimu waliyotoa na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari kuhusu uvutaji wa sigara katika maeneo yasiyo rasmi.
Source: Nipashe
loswahili ni kibantuDah.....wabongo wanajichanganya kweli....sugars siyo bangi Wala sex....Kuna tofauti kati ya hadhara....na hadharani....hadhara ni sehemu yenye mikusanyiko ya watu Kama masokoni, vituo vya Basi, kumbi za starehe nk.....na hadharani ni sehemu yoyote ambayo mtu anaonekana na mtu mwingine...hata ukikaa barazani kwako uko hadharani.....ukiwa shamba kwako nk.....tutafautishe kati ya maeneo ya umma.....maeneo ya wazi.....na maeneo binafsi....bila hivyo tamko hili Ni upuuzi🤣🤣🤣🤣🤣
Dah....kwa tamko hili maana yake Ni sawa na kupiga marufuku uvutaji wa sugars 🤣🤣🤣🤣🤣🤣wavutie wapi sasa
sigara ndo kodi yenyewe sasa wachana na hizi tozoDah....kwa tamko hili maana yake Ni sawa na kupiga marufuku uvutaji wa sugars 🤣🤣🤣🤣🤣🤣