Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Baada ya Mdau kuandika hoja kuhusu Viongozi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) akidai wanakaa madarakani kwa muda mrefu bila ukomo wa wazi, hali inayopunguza uwakilishi na kuzuia mawazo mapya na baadhi ya Wataalamu kuhisi kukosa sauti ya ushiriki katika maendeleo ya taaluma yao, Baraza hilo limetoa ufafanuzi.
Hoja ya Mdau ~ Uongozi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) uwe na ukomo. Miaka yote Viongozi walewale, hawataki mawazo mbadala
Tanzania Nursing and Midwifery Council lina jukumu la kuhakikisha kuwa wauguzi na wakunga wanatoa huduma salama, bora na zinazokidhi viwango vya taaluma.
TNMC si chama kama mtoa mawazo anavyodai TNMC inafanya kazi kwa mujibu wa sheria ilitungwa na Bunge la Jamhuri na si katiba kama mdau anavyodai, TNMC inaongozwa na wajumbe wasiopungua 12 ambao wanateuliwa na mhe. Waziri wa Afya kwa mujibu wa Sheria ya Uuguzi na ukunga na wadumu madarakani kwa muda wa miaka mitano tu.
Nje ya sekretarieti wengine wanaoajiriwa kwa mujibu wa miongozo ya kiutumishi kama watumishi wengine wa umma wanavyoajiriwa.
TNMC ipo kwaajili ya kuhakikisha jamii inapata huduma bora za uuguzi na ukunga si vinginevyo.
Hoja ya Mdau ~ Uongozi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) uwe na ukomo. Miaka yote Viongozi walewale, hawataki mawazo mbadala
TAARIFA YA BARAZA
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) ni chombo cha kisheria kilichoanzishwa na Serikali ya Tanzania kusimamia taaluma ya uuguzi na ukunga nchini.Tanzania Nursing and Midwifery Council lina jukumu la kuhakikisha kuwa wauguzi na wakunga wanatoa huduma salama, bora na zinazokidhi viwango vya taaluma.