Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Don; umefanya vizuri kuwa na wazo la kutafuta kazi ili usipoteze muda wakati unasubiri majibu; ushauri wangu usitafute kazi ya malipo (Temporary Employment), maeneo mengi ya kazi hayana upungufu wa namna hiyo hata kuamua kuweka form 6 leavers kazini, hayo mambo yalikuwepo miaka ya 70 ambapo kulikuwa hakuna wataalamu wa kutosha. Bado kuna idadi ya wengi wenye taaluma kutoka vyuo mbalimbali wanatafuta kazi, japokuwa hii haiwezi kuwa kigezo cha wewe kukosa kazi.
Hivyo basi badala ya kutafuta kazi ya kulipwa ningekushauri utafute kazi ya kufanya bila malipo (VOLUNTEER)
VOLUNTEER Ni Kutoa/kutumia muda wako katika kufanya mambo/jambo ambalo litakuwa na manufaa, lakini bila kutegemea ujira wowote.
FAIDA ZAKE:
Kutumia muda na nguvu zako vizuri
Kukutana na watu tofauti/mbalimbali
Kujifunza kwa njia ya vitendo (learning by doing)
Kuhudumia wengine au jamii inayokuzunguka
Kwa wale wote ambao wanatafuta kazi, tumia fursa hii..(VOLUNTEER)
Ushauri wangu tu ndugu, ingawa wengi watabisha hapa (nimegundua hili kwa muda mdogo niliojiunga, kuna watu ubishi ni kazi yao) kwanza soma tena barua yako, kuna makosa mengi mno ya uchapishaji. Umechanganya maneno mengi mfano Applicationfor, Schoolseeking, KiswahiliandComputer, supervision,to ni makosa madogo madogo, lakini kama wewe ndie unaepokea barua namna hii hivi kweli utamuajiri mhusika? Mimi sitokuajiri kwa sababu unaonyesha dhahiri kuwa utakuwa ukifanya makosa kazini, na pia huko serious kwa sababu kama uko serious ungelichukua muda kusoma barua yako kutoa makosa kabla ya kuituma.
Pia kwenye strong attributes, ok ndio kwanza umemaliza form six, lakini ushahidi wa unayosema uko wapi? ningelikushauri ure-phrase sentensi hiyo na uweke ushahidi, maneno kamam possessing proven x and y skills as proven by completing/assisting/etc.
I have a good command in English, Kiswahili and Computer Literacy. sentensi hii unadhani iko sawa? good command in cumputer literacy? really? by the way it is swahili and not kiswahili. Kumbuka Ki tunatumia kuashiria aina ya lugha na sio sehemu ya jina la lugha; kiarabu, kifaransa, kifini, kijapani etc.
Ningelikushauri ure-phrase ulivyoanza barua yako pia "I am a form six leaver of the year 2012 from" iandike kivyengine.