E, Kloro muungwana, hakika umenishtua
Vipi asili wakana, kwa mambo ya vitumbua
Humuogopi maulana, dunia inazuzua
usasa una mashaka, ndugu yangu tahadhari
usemalo si la mana, ndugu wanihuzunisha
Tigo kitu ya laana, leo nakuhabarisha
Imekatazwa na rabana, mbona mwaihalalisha
usasa una mashaka, ndugu yangu tahadhari
Duniani tuwe wema, tusimuudhi rabuka
umalaya si jambo jema, vipi akighadhibika
Tutakosa pa kushika, mola kileta gharika
Usasa una mashaka, ndugu yangu tahadhari
Ya dunia sitamani,bora niitwe mshamba
vipi nijivue thamani,nichane wangu msamba
Mengi ya sasa huzuni, twajigongeza na mwamba
usasa una mashaka ndugu yangu tahadhari
Na kama nimekukwaza, naomba niwie radhi
Ni wajibu kukukataza, tuyaepuke maradhi
Wengine wayasambaza, kweli hatuna hadhi
usasa una mashaka, ndugu yangu tahadhari
QUOTE=.
[/QUOTE]
Ndugu yangu yakuonea, umenisoma visivyo
Yote nilioongea , ndo hali ya sasa ilivyo
Wala sikukusudia, namimi naamini hivyo
Sitojitwika dunia , kuiga mambo ya ovyo
Ninaloamini ni moja, kati ya orodha yangu
Uongo ni wenye tija, mapenzini ni chachandu
Hili limejaa hoja, kiswahili na kizungu
mengine niloyataja, yawahusu walimwengu.
Tukubali tukatae , hili janga tuko nalo
Hata vikao tukae, hatulipunguzi kilo
Tukisema tukimbie, labda tuende selo
Tukiamua tulie , zitalowana taulo
Nakubali ulonena, kuhusu hayo ya tigo
Ni kweli yana laana, si mema hata kidogo
Lakini yangu maana, tuukubali mzigo
Ukitaka kusonona, utaumiza mafigo.
Amini unavyoamini, uishi maisha yako
Wa sasa utamaduni, kuubadili ni mwiko
Wenyewe wauthamini, twaonekana vituko
watuita wa sabini , tukihoji machafuko.
Wala hukunikwaza, hiyo hofu iondowe
Nahisi umenikweza, kunifanya nielewe
Bado nimo najifunza, mwalimu usichelewe
Shairi si ukewenza, liweke tulichambuwe