We Wizzy,watu watatia shaka hata wazo lako.
We mtu atakujaje bila kujua wazo lako ni lipi na mtaji kiasi hani.Maana hakuna business Plan yoyote duniani ambayo haijulikani,tofauti inakuja tu kwenye sehem husika,muda husika,matarajio husika,na mazingira husika
Halafu kwa kukusaidia tu,mfumo huo hauwezi ku apply,sio kwamba nakukatisha tamaa,lakini presentation yako tu tayari ni loss,sasa hiyo biashara si itakuwa super loss business?
Muungwana hapo juu kakuuliza kwanza tu mtaji bado hujamjibu,yaani hata hili nalo gum?
Pia wapo watu wataotaka dhamana,maana kama unachukua 20% of net profit ni kwamba umeingia kwenye hisa kwa kuuza wazo.Haalfu unasema kwamba miaka minne akuachie.
Hii ndio imenichekesha kweli,yaani wabongo tumekaa kitamaa tamaaaaa
Kuna watu humu wana miaka 15 wanaendesha Daladala moja Gobole,Gobole hilo limeisha nunua Coaster karibia 7,lakini hata siku moja tajiri hajasema Dereva hembu chukua liwe lako.
Biashara yoyote yenye plan ya long time returns huwezi kuipa period ya miaka minne kuwa stable.
Fikiria kitu kingine twende kibaha tukalime,