Toa ushauri kwa kocha wa Simba timu iwaje.

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Watu wengi wanamlaumu sana Kocha wa Simba jinsi anavyopanga timu na chaguo la wachezaji anaowachezesha kipindi cha kwanza au cha pili.

Shutuma ya pili ni mbinu za kimchezo anazotumia Kocha huyo. Kuna watu wanaona Simba inacheza kimparaganyiko na taratibu sana.

Jee Kocha Roberthino afanye kitu Gani kuifanya Simba iwe Bora zaidi kuliko sasa!!??
 
Yaani mashabiki mtoe ushauri jinsi gani kocha apange kikosi chake[emoji848][emoji848]?
Rage alikuwa sahihi kuwaita mbumbumbu[emoji23][emoji23]
Unapolaumu si lazima uwe na suluhisho? Wanaosema anakosea kupanga kikosi si waseme kikosi kiweje?

Hii ni Mantiki ya kawaida kabisa!!
 
Wengi wa hao wanamlaumu kocha mpira wameujulia kwa kusikiliza kwenye radio hivyo hawana akili ya maboresho wao wamekaririshwa kulaumu tu.
 
Mdogo mdogo kocha anaanza kubadilika, Angalau ameanza kupanga kikosi kinachoeleweka, lkn pia anawapa nafasi na wengine kucheza ktk gemu ambazo zinaonekana hazina changamoto kubwa.
 
Baada ya Moses Phiri aliyekuwa akililiwa kupewa nafasi, na kuishia tu kuruka ruka uwanjani! Sasa hivi mashabiki wamekuja na kilio kingine cha kutaka rotation eti kwenye timu!

Wanataka kila mchezaji aliyesajiliwa acheze kama wafanyavyo Yanga!! Sasa jiulize hawa mashabiki wanajielewa kweli? Hivi kikosi cha Yanga ni cha kujilinganisha nacho kweli? 😇
 
Kocha atoe nafasi kwa wachezaji wore waliosajiliwa, awe anafanya mabadiliko mapema, ajue utamaduni wa mpira wa Simba ni kuweka mpira chini na sio butubutu. Awape nafasi wenye energy sio mchezaji amechoka au anajua kabisa hawezi kucheza dakika 90 anamng'ang'ania.
 
Fukuza kocha, lete Julio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…