Uchaguzi 2020 Tofauti kadhaa kati ya Lowassa (2015) na Lissu (2020)

Uchaguzi 2020 Tofauti kadhaa kati ya Lowassa (2015) na Lissu (2020)

Tall Guy fam

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2017
Posts
917
Reaction score
1,093
Bila kupoteza muda

1. Lowassa alikuwa delusional, nikimaanisha alikuwa anaamini atachukua nchi asubuhi na mapema hii ni kwa sababu alikuwa na "marafiki" kila sehemu.
Lissu yeye kwa maneno yake anaamini kinyume chake kwamba Uchaguzi utakua mgumu, usio huru na haki hivyo ni lazima wajipange.

2. Wakati Lowassa aliamini tume ya taifa ya Uchaguzi itamtangaza kuwa yeye ndiye mshindi pengine alikua na "marafiki" humo, Lissu yeye hatarajii hilo kutokea. Inaonyesha yeye anawaza zaidi kutumia njia mbadala endapo ataporwa ushindi.

3. Lissu anajua vizuri haki zake, sheria na katiba ya nchi tofauti na Lowassa, kitu ambacho kinamsaidia kuvuka viunzi mbali mbali vya tume, msajili na serikali kwa ujumla katika kipindi cha Uchaguzi.

4. Lowassa alikuwa na vingi vya kupoteza, biashara, familia etc. hivyo ni rahisi kuunga mkono juhudi ili kuvilinda. Lissu hana chochote cha kupoteza, amejitoa mazima. Katika moja ya mahojiano alisema yeye anachowaza ni kama baada ya Uchaguzi atakua hai.

5. Lowassa aliposhindwa alikubali matokeo. Lissu, kama uchaguzi utakuwa na kasoro, usio huru na haki, viashiria vyote vya kuibiwa kura n.k HATOKUBALI. Ninaamini yeye binafsi atakuwa mstari wa mbele katika maandamano ya kudai haki.
 
Back
Top Bottom