Tofauti kati ya computer science na IT

Mimi na muhitimu wa Shahada ya kwanza katika sayansi ya kompyupa. Mimi ninachofahamu ni kwamba

Bsc in Computer Sc, Bsc in IT.

Mfano:
University of Dar es Salaam
Bsc in Cmptr sc ni lazima awe amesoma Physics na Math (PCM, PGM) na darasa wanafunzi hufunzwa Mathematics pia mwaka wa kwanza mpaka wa mwisho.

Institute of Financial Management(IFM)

IT.
Mwanafunzi yoyote aliye soma masomo ya sayansi O-level au A-level anaruhusiwa kusoma IT. Math sio somo la lazima mwaka wa kwanza mpaka wa mwisho.

Naomba niishie hapa ntarudi ili niweke full documents kuonesha tofauti
 

Sio kweli... IFM ili mtu usome computer science au IT Math ni somo la lazima na uwe umefaulj pia lazima uwe umesoma pure science subjects bila hivyo labda uwe umeanza certificate ukaja diploma ndo ukaingia degree. Bila hesabu hayo masomo hayaendi. Kuna binary caliculation Quantitative mathematics na mengine so usidanganye mtu yoyote kua maths si la lazima
 

Sio lazima usomee PCM and PGM hili usome computer science. Mwanafunzi anaweza kutoka O level na kwenda moja kwa moja kuchukua degree yoyote ikiwemo ya computer science.

Kuwa na PCM au PGM ni criteria zilizowekwa na UDSM na vyuo vya Tanzania. Lakini sio muhimu katika masomo ya computer science.

Kuhusiana na maana ya degree zenyewe. Zamani kulikuwa hakuna degree ya computer science. Mpaka sasa pioneers wa computer science ni watu waliosomea electrical engineering, mathematics, material science and physics. Kwa miaka mingi ilikuwa ni sehemu ya department ya Electrical Engineering or Mathematics. Mwishoni mwa miaka ya 80 na mwanzoni 90 kulikuwa na ongezeko kubwa la matumizi computers na mahitaji ya wataalamu yaliongezeka. Hivyo vyuo vingi vilianzisha department ya computer science kupata wataalamu na watafiti.

Katika miaka ya 90 matumizi ya computer na telecommunication yaliongezeka zaidi na kwenye fani mbalimbali. Na vilevile kukaanza kutokea wataalamu wa matumizi ya computer katika fani hizo. Huu ndio ujio wa IT. Hivyo mtu kuwa mtaalamu wa IT sio lazima awe amebobea sana kwenye maths. Inategemea anatumia applications za computer kwenye masuala gani. Matokeo ya utafiti yaliyofanyika miaka ya nyuma yamefanya matumizi ya applications za computer kuwa user friendly.

Kuhusiana na Software Engineering, hii inahusiana na development ya software. Miaka ya zamani computer programmers walikuwa wana-develop programs au applications kwa kufuata utaratibu waliojipangia. Hii ilisababisha gharama za ku-maintain na ku-develop software kuwa kubwa na process kuwa unpredicatability. Hivyo wataalamu wakaamua kutumia mbinu zinazotumika kwenye fields zingine za engineering kuboresha development of software. Kwa mfano kwenye utengenezaji wa magari kuna designer, kuna mechanical engineer, kuna interior designer na watu wengine. Watu hawa wanafanya kazi katika sehemu tofauti na kwa vipindi tofauti lakini wanakuletea kitu cha mwisho chenye kueleweka kwa sababu wanatumia proven methodologies kupata matokeo.

Hivyo kuwa software engineer sio lazima usomee software engineer. Ukiwa unashiriki katika sehemu muhimu za software development life cycle na kufuata proven methodologies, wewe tayari ni software engineer.

Kuna mtu kagusia informatics. Ukiondoa UK, Ireland and Scotland, nchi nyingi za Ulaya zinatumia informatics kama computer science. Wanaosomea wanachukua masomo yote ya computer science.

Kuhusiana na computer engineering, hapa inahusiana na mambo ya computer hardware. Na vilevile wanaochukua CE wanachukua masomo mengi ya computer science.

Kwa ujumla wenye mafanikio mazuri kwenye masuala ya computer ni wale wenye kutumia vipaji na wenye passion. Kuwa na degree inakupa profile tu lakini haikusaidii kama huna talents na passion.

Wenu

Z-10
 

Umenena mkuu watu wengi niliosoma nao walikua wazuri kwenye theory lakina ukimpeleka lab anaona mataa taa mtu anasoma tu ilmrad degree atulie. Afu watu wanaotengeneza computer mtaani wanajiita wana it hata kama hawajasoma chuo chochote. Wanadhani it ni kuinstall windows na kuchoma motherboard peke yake. Hawajui hayo masomo ni wide kuna vitu kama programming maintanance and repair web technologies zdatabase development software engneering system analysis and design etc........
 
habari zenu wadau,

hivi hii course ya busines information system (BIT) ina kuwa na sifa gani kujiunga nayo? mi nimesoma HGE, nataka nije niisome baadae kwa faida yangu binafsi!
 
kwahiyo mtu wa EGM hawezi soma IT pale UDSM ?
 


Mkuu Ezless umesema ki2 kizuri sana (BIT) naitafta kila kona,,ni chuo gani kinatoa masters of Bussiness Information Technology????
 
habari zenu wadau,

hivi hii course ya busines information system (BIT) ina kuwa na sifa gani kujiunga nayo? mi nimesoma HGE, nataka nije niisome baadae kwa faida yangu binafsi!

Tanzania kuna complications kidogo au nyingi kuhusiana na sifa za kujiunga na fani zakusomea. Katika nchi zenye nafasi nyingi, kinachokupeleka kusomea ni aptitude yako na sio PCM au PCB.
 

Unawezakuona kuwa unadharauliwa kwa sababu mtu anasema ukweli. Mfumo wa elimu wa Tanzania unachangia kwa kiasi fulani. Watu wanasoma kwa combination za A level. Lakini sio kwa mapenzi.

Vilevile ni lazima kuwepo na ajira zinazo-support. Sijuhi kama mambo yamebadilika. Lakini nilipokuwa bongo miaka ya zamani, makampuni mengi ya bongo yalikuwa yana-subcontract kazi zao kwa makampuni yaliopo India au Dubai. Hii ilifanya talents za Tanzania kufanya kazi za support na sio software development.
 

IT ni mwavuli mkubwa wenye kujumlisha watu wenye fani nyingi. Ana-repair computers nao wapo kwenye IT. Kuanzisha kampuni yako na kazi yako ikawa ni kusaidia makampuni kuingiza data za mishahara ya wafanyakazi wao kwenye computers, utakuwa kwenye IT - data entry.

Kutokana na maelezo katika posti nyingi hapa, inaonyesha watu wawe wanataka kutambulika kwa vile walivyosomea. Ukweli wa mambo katika masuala ya computer, aptitude and talent ndio vitu muhimu.
 
Unawezakuona kuwa unadharauliwa kwa sababu mtu anasema ukweli. Mfumo wa elimu wa Tanzania unachangia kwa kiasi fulani. Watu wanasoma kwa combination za A level. Lakini sio kwa mapenzi.
Ni kweli tuna mfumo wa elimu usio mzurni na bahati mbaya wanasiasa wanazidi kuuharibu. Lakini hii haimpi uhalali wa yeye kutudharau Watanzania (na sio mfumo wa Tanzania). Ninawajua watu wazuri katika fani hii kupita huyu ndugu na nin hakika tukiweka challenge watamtoa knock out.

Mambo yamebadilika kwa wananchi kuamka na kuanza kufanya yale Makampuni haya yalikuwa yakifuata huko India. Bado Makampuni mengi hayajawaamini Wazalendo ila kwa trend hii ndiko tunakoelekea.

Tatizo letu ni kulaumu serikali badala ya kupigania fursa hata finyu tulizo nazo. Ila vijana wengi wameamka na inatia moyo. Hope Serikali itaacha kutoa kila fursa kwa wageni bali itawasaidia wazalendo kuweza kuzitumia fursa hizo kwa maslahi ya Taifa hili!
 
bizness information systems.....hii kitu safi sana

wakuu mimi nilisoma Bsc Software Engineering pale udom, potential yake ni kubwa sana kwa tanzania hasa kama unataka kujiajiri mwenyewe au kuwa mjasiriamali kwajili ya masoko madogomadogo. nilipata bahati pia ya kufanya training katika makampuni makubwa mawili ya hapa nikagundua kuwa makampuni hayo huwa yanaagiza software zote nje na software hizo sio mpya zinakuwa updated tu kuminimise risk and any other security threat. sasahivi ninasoma business information technology hapa daressalaam na inaonekana wazi ni jinsigani makampuni yanahitaji ict staff wenye knowledge ya business ili kuepuka mzigo wa ict staff ambao hawazalishi direcly nikimaanisha wao kufanya kazi ni mpaka tatizo litokee.
 
du mie simo hayo ni majanga ajira kwa fani yoyote ya computer ni ngumu kwa sasa tz coz ni fani ambayo mtu mwenye ujuzi mwingine tofauti anajiendeleza kwa hiyo makampuni mengi yanaamua ku update wafanyakazi wao kuliuko kuajiri new employee kilichoimaliza hiyo fani ni zile coz hadi za mwezi mmoja plus utundu tayari anaweza
 
dah, yaani pamoja na mkuu Jorzy kuongea some facts lakini wewe umetafuta vikosa vidogo na kukomalia hapo??

mmhh!!
Nafikiri hii fani unaionea kwa mbali sana, kwani ungeifahamu ungeona kwa nini watu wanakataa hoja za Jorzy hapo juu. Akili ni nywele....Miye namshangaa Jorzy, wewe wanishangaa miye na miye nakushangaa wewe.....
 
mkuu fadhili paul nimekuelewa shukrani kwa ufafanuzi lakini kwa mazingira yetu africa ipi inakuwa ni nzuri kusoma na linapokuja suala la ajira ipi ni nzuri.

Ajira upande gani?
self-employment au ile ya kuajiriwa na NGOs na GOs?
kama ni self-employment wala hamna shida
lkn kama unasoma hizi course uje kuajiliwa umepotea lazima ujipange "education for self-reliance"
 

Change your mentality and things are going to be okay!
Kama hawataki kukuajiri, Jiajiri ili uje uajiri waliokosa ajira!
 

Inaonekana umeingia mahali uka select all kisha copy then uka paste Mzigo kama ulivyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…