chotarasukari
Senior Member
- Jan 6, 2013
- 110
- 23
Sio lazima usomee PCM and PGM hili usome computer science. Mwanafunzi anaweza kutoka O level na kwenda moja kwa moja kuchukua degree yoyote ikiwemo ya computer science.
Kuwa na PCM au PGM ni criteria zilizowekwa na UDSM na vyuo vya Tanzania. Lakini sio muhimu katika masomo ya computer science.
Kuhusiana na maana ya degree zenyewe. Zamani kulikuwa hakuna degree ya computer science. Mpaka sasa pioneers wa computer science ni watu waliosomea electrical engineering, mathematics, material science and physics. Kwa miaka mingi ilikuwa ni sehemu ya department ya Electrical Engineering or Mathematics. Mwishoni mwa miaka ya 80 na mwanzoni 90 kulikuwa na ongezeko kubwa la matumizi computers na mahitaji ya wataalamu yaliongezeka. Hivyo vyuo vingi vilianzisha department ya computer science kupata wataalamu na watafiti.
Katika miaka ya 90 matumizi ya computer na telecommunication yaliongezeka zaidi na kwenye fani mbalimbali. Na vilevile kukaanza kutokea wataalamu wa matumizi ya computer katika fani hizo. Huu ndio ujio wa IT. Hivyo mtu kuwa mtaalamu wa IT sio lazima awe amebobea sana kwenye maths. Inategemea anatumia applications za computer kwenye masuala gani. Matokeo ya utafiti yaliyofanyika miaka ya nyuma yamefanya matumizi ya applications za computer kuwa user friendly.
Kuhusiana na Software Engineering, hii inahusiana na development ya software. Miaka ya zamani computer programmers walikuwa wana-develop programs au applications kwa kufuata utaratibu waliojipangia. Hii ilisababisha gharama za ku-maintain na ku-develop software kuwa kubwa na process kuwa unpredicatability. Hivyo wataalamu wakaamua kutumia mbinu zinazotumika kwenye fields zingine za engineering kuboresha development of software. Kwa mfano kwenye utengenezaji wa magari kuna designer, kuna mechanical engineer, kuna interior designer na watu wengine. Watu hawa wanafanya kazi katika sehemu tofauti na kwa vipindi tofauti lakini wanakuletea kitu cha mwisho chenye kueleweka kwa sababu wanatumia proven methodologies kupata matokeo.
Hivyo kuwa software engineer sio lazima usomee software engineer. Ukiwa unashiriki katika sehemu muhimu za software development life cycle na kufuata proven methodologies, wewe tayari ni software engineer.
Kuna mtu kagusia informatics. Ukiondoa UK, Ireland and Scotland, nchi nyingi za Ulaya zinatumia informatics kama computer science. Wanaosomea wanachukua masomo yote ya computer science.
Kuhusiana na computer engineering, hapa inahusiana na mambo ya computer hardware. Na vilevile wanaochukua CE wanachukua masomo mengi ya computer science.
Kwa ujumla wenye mafanikio mazuri kwenye masuala ya computer ni wale wenye kutumia vipaji na wenye passion. Kuwa na degree inakupa profile tu lakini haikusaidii kama huna talents na passion.
Wenu
Z-10
Nimekuelewa sana kwa maelezo yako. vip upande wa networking hesabu lazima uijue?