Zipo gari nyingi tu ambazo ni full time 4wd tangu zamani mfano ni land rover 110 nadhani pia subaru tangu enzi hizo. Kila mfumo una uzuri/faida na ubaya/hasara zake kwenye matumizi ya kila siku. Nitatoa mfano nilishakuwa na land cruiser HJ60 miaka ya 90 halafu na pia land rover 110 katika mizunguko ipo siku cross joint ilikufa ktk cruiser porini huko Mvuti, nikafungua propeller nikaunga front wheel nikarudi mjini na ikatokea pia ktk 110 ilibidi kuvutwa tu, ukitoa propeller mwisho wa taarifa ya habari