Nisaidieni nifahamu kutofautisha injini....
3L, 1HZ, 1KZ n.k maana yake nini?
Hizo ni injini za Diesel za Toyota. Toyota wao injini zao za diesel wamezipa code kuonyesha injini ina idadi gani ya cylinder.
Baadhi ya Kodi za diesel injini ni B,G,H,L,V
. Kwa Toyota wao Kwanza inaanza namna kisha herufi baada ya hapo ukikuta mkato kisha herufi F-Fuel injection na T-Turbo hizi huwa mwisho kuonyesha injini ina mfumo wa fuel injection na T inaonyesha gari ina turbo.
Tuje kwenye 3L,1KZ,1HZ. L hizi injini zipo L,2L,3L na 5L. L injini hii ilitumika kwenye sedan kama Mark na Chaser matoleo ya Zamani. 2L hii imetumika kwenye Toyota Hilux,Hiace, Surf Sana tumeiona kwenye Hilux za Zamani na 2L ina 2400cc ubavuni hizi gari zilikuwa na chata ya 2.4L kuonyesha ina 2400cc.
3L hii ni injini yenye 2800cc na imetumika kwenye Toyota Hilux,Hiace,Surf,Prado, Fortuner na Surf kwenye baadhi ya hizi gari utakuta kuna Lebo wameweka ya 2.8L.
5L injini hii ina 3000cc nayo imetumika kwenye Toyota Hilux,Hiace, Fortuner na huonyeshwa Kwa Alama ya 3.0L au D3.0.
Kwenye hizi injini ukikuta 2L au 3L hii ni natural aspirated engine haina turbo Ila ukikuta ina code 2L-T au 3L-T hii ina turbo.
1KZ hii ni injini ya Toyota ya diesel ambavyo imetumika kwenye Toyota Hilux,Hiace,Surf, Prado hii ina 3000cc. Ukikuta ina code hii 1KZ-T hii herufi T inakuonyesha injini hii ina turbo. Hii ilikuja baada ya Injini za L ikiwa ni maboresho Zaidi na baada ya 1KZ ikaja 1KD na 2KD ambazo bado zilifungwa katika Hiace,Prado na Hilux. Kisha imekuja kufunga kazi 1GD-FTV ambayo ipo kwenye Prado za sasa na Hilux hii imekuwa maarufu kutokana na watu kupenda tone ya ule mluzi wa turbo.
1HZ hii ni injini kongwe, roho ya paka na yenye nguvu iloyotengenezwa na kuwekwa kwenye Toyota Land Cruiser series 70/80, Toyota Coaster ambazo utakuta zina chasisi yenye code ya HZJ*****.Hii ni injini yenye 6cylinder na 4200cc au 4.2L injini hii imetengenezwa bila turbo. Ila Toyota kuna baadhi ya Coaster injini hizi za 1HZ walizitengeneza na turbo hivyo zikawa zimekuja na code ya 1HZ-T, kwenye Land Cruiser ukikuta 1HZ-T jua imefanyiwa modifications.
Tofauti ya hizi injini ambayo ni nyepesi ni kuwa 3L ina 2800cc na 4 cylinder ,1KZ ina 3000cc na ni 4 cylinders, 1 HZ ina 4200cc na ni inline 6 cylinders.Hapo utaona ipi ni kubwa,yenye nguvu na muungurumo wa kibabe kuzidi mwenzie.
Adiós Amigo