Tofauti kati ya Land Cruiser Prado na Land Cruiser isiyo Prado

Tofauti kati ya Land Cruiser Prado na Land Cruiser isiyo Prado

Sasa kama vimashine vya yamaha havina hata horsepower 50 uje ufunge mashine yenye horsepower 134 huoni kama show inakuwa kali.
zile boti za utalii au ndogo za uvuvi HP 75 ni mwisho.
nizo boti za zannzibari ndo mitaa yake iyo.
imagine meli kata titaniki engine. 6 si chin ya hp46000
engine boen twinejet zina hp 175000
 
zile boti za utalii au ndogo za uvuvi HP 75 ni mwisho.
nizo boti za zannzibari ndo mitaa yake iyo.
imagine meli kata tikaniki engine. 6 di chin ya hp46000
engine boen twinejet zina hp 175000
Hahahah hizo horsepower ni balaa,
 
Hizo ni injini za Diesel za Toyota. Toyota wao injini zao za diesel wamezipa code kuonyesha injini ina idadi gani ya cylinder.

Baadhi ya Kodi za diesel injini ni B,G,H,L,V
. Kwa Toyota wao Kwanza inaanza namna kisha herufi baada ya hapo ukikuta mkato kisha herufi F-Fuel injection na T-Turbo hizi huwa mwisho kuonyesha injini ina mfumo wa fuel injection na T inaonyesha gari ina turbo.

Tuje kwenye 3L,1KZ,1HZ. L hizi injini zipo L,2L,3L na 5L. L injini hii ilitumika kwenye sedan kama Mark na Chaser matoleo ya Zamani. 2L hii imetumika kwenye Toyota Hilux,Hiace, Surf Sana tumeiona kwenye Hilux za Zamani na 2L ina 2400cc ubavuni hizi gari zilikuwa na chata ya 2.4L kuonyesha ina 2400cc.

3L hii ni injini yenye 2800cc na imetumika kwenye Toyota Hilux,Hiace,Surf,Prado, Fortuner na Surf kwenye baadhi ya hizi gari utakuta kuna Lebo wameweka ya 2.8L.

5L injini hii ina 3000cc nayo imetumika kwenye Toyota Hilux,Hiace, Fortuner na huonyeshwa Kwa Alama ya 3.0L au D3.0.
Kwenye hizi injini ukikuta 2L au 3L hii ni natural aspirated engine haina turbo Ila ukikuta ina code 2L-T au 3L-T hii ina turbo.

1KZ hii ni injini ya Toyota ya diesel ambavyo imetumika kwenye Toyota Hilux,Hiace,Surf, Prado hii ina 3000cc. Ukikuta ina code hii 1KZ-T hii herufi T inakuonyesha injini hii ina turbo. Hii ilikuja baada ya Injini za L ikiwa ni maboresho Zaidi na baada ya 1KZ ikaja 1KD na 2KD ambazo bado zilifungwa katika Hiace,Prado na Hilux. Kisha imekuja kufunga kazi 1GD-FTV ambayo ipo kwenye Prado za sasa na Hilux hii imekuwa maarufu kutokana na watu kupenda tone ya ule mluzi wa turbo.

1HZ hii ni injini kongwe, roho ya paka na yenye nguvu iloyotengenezwa na kuwekwa kwenye Toyota Land Cruiser series 70/80, Toyota Coaster ambazo utakuta zina chasisi yenye code ya HZJ*****.Hii ni injini yenye 6cylinder na 4200cc au 4.2L injini hii imetengenezwa bila turbo. Ila Toyota kuna baadhi ya Coaster injini hizi za 1HZ walizitengeneza na turbo hivyo zikawa zimekuja na code ya 1HZ-T, kwenye Land Cruiser ukikuta 1HZ-T jua imefanyiwa modifications.

Tofauti ya hizi injini ambayo ni nyepesi ni kuwa 3L ina 2800cc na 4 cylinder ,1KZ ina 3000cc na ni 4 cylinders, 1 HZ ina 4200cc na ni inline 6 cylinders.Hapo utaona ipi ni kubwa,yenye nguvu na muungurumo wa kibabe kuzidi mwenzie.

Adiós Amigo
Mkuu umefafanua vyema sana ila marekebisho kidogo hapo kwenye 1HZ badilisha ni CC 4160 pia umesahau 1C au injini za code C ambazo ni dizeli na huja na Chasser mark II sedan
 
gari ni kadude kadogo sana max hp ipo kwenye gari inaitwa regera hp 1460 still watu wana vitz za hp 70🤣🤣
Hahahahahah sahizi wajerumani wengi wako kwenye threshold ya 400-600HP kwenye top spec ya practical cars. Humo ni kwa kujaza ma turbo turbo chargers.

Mjapani ndio yuko kati ya 200-400
 
zile boti za utalii au ndogo za uvuvi HP 75 ni mwisho.
nizo boti za zannzibari ndo mitaa yake iyo.
imagine meli kata titaniki engine. 6 si chin ya hp46000
engine boen twinejet zina hp 175000
Hizo hp za meli zisikutishe mkuu sababu zinaendana na uzito wake!

Emma Maersk ina 108920 hp lakini top speed ni 55 km/h!!
 
Back
Top Bottom