Frumence M Kyauke
JF-Expert Member
- Aug 30, 2021
- 630
- 1,262
Watu wengi wanashindwa kutofautisha kati ya mhuni na mhalifu na kuleta mkanganyiko pale wanapotaka kufahamu tofauti ya watu hawa wawili.
Mhuni ni mtu yeyote aliyeamua kwenda kinyume na maadaili mema au utamaduni huku mhalifu ni mtu yeyote aliyevunja sheria.
Mhuni anakosa maadili mema na kufanya mambo yanayokinzana na tamaduni za watu anaoishi nao iwe jamii au nchi kwa ujumla.
Mhuni anaweza kuwa anatumia mihadarati, kauli chafu, anavaa mavazi yasiyo na staha, mitindo mibovu ya urembo wa mwili wake, mtu muongo, mtu anayejihusisha na ushoga au usagaji kwa kuridhia mwenyewe, kwa ujumla mtu asiye mcha Mungu
Mhalifu yeye anafanya makosa yaliyokatazwa katika sheria iliyowekwa ikiwemo wizi, uuaji, ubakaji, utakatishaji wa fedha, biashara haramu, udhalilishaji kwa njia yeyote ile, na mengineyo.
Mhuni anaweza asiwe mhalifu hii inatokea pale anapokosa maadili kama kutokwenda kwenye ibada, mitindo mibovu ya mavazi, kukosa heshima, uvivu, uchafu wa mwili na mazingira yanayomzunguka lakini havunji sheria za nchi.
Mhalifu anaweza asiwe mhuni hii inatokea pale mhalifu huyu kuwa na maadili yanayopendeza jamii yake au nchi yake anapokuwa mbele za watu lakini anatekeleza uhalifu kwa njia ya siri sana na watu wasimtambue kuwa ni mhalifu.
Ni rahisi sana kumtambua mhuni kuliko mhalifu kwasababu mhuni anaonekana kuwa amekosa maadili lakini mhalifu anaweza asitambulike kwa haraka ikiwa anavunja sheria akiwa peke yake au kwa siri.