Tofauti kati ya mvulana na mwanaume

Tofauti kati ya mvulana na mwanaume

CARIFONIA

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2013
Posts
616
Reaction score
1,453
"Endapo bado hujaelewa tofauti kati ya wavulana na wanaume, hapa kuna mifano michache inayohusu mahusiano ya kimapenzi:

- Mvulana: hutumia wanawake kujenga kujiamini.
Mwanaume tayari ana kujiamini.

- Mvulana: hupenda 'kudate' tu na mwanamke anayemvutia.

-Mwanaume: humualika kwenye miadi rasmi.

Mvulana: husubiri hadi awe na uhakika kuwa hakuna hatari kabla ya kuchukua hatua.
Mwanaume: ni jasiri na hufanya maamuzi wazi kuhusu nia yake.

- Mvulana: hucheza michezo ya kihisia na mwanamke.

Mwanaume: hana muda wa michezo hiyo kwa sababu inamzuia kumjua mwanamke kwa undani.

- Mvulana: hujawa na hasira na kinyongo mwanamke anapomkataa.

Mwanaume: hukubali kuwa mahusiano yanahusisha hatari ya kukataliwa.

- Mvulana: huwa na hofu au huabudu wanawake.

Mwanaume: huheshimu na kuwathamini wanawake, lakini huogopa na kumwabudu Mungu pekee.

- Wavulana: ni baridi na wasiojali.
Wanaume: ni wenye shauku na ari kubwa."
 
Hii tafsiri ya mwanaume na mvulana , mara nyingi hutumiwa na wadada wa mjini kuwaseti vijana ili wawe watumwa wao.

Mvulana ni mtoto wa kiume ambae bado hajafikia umri wa utu uzima.

Mwanaume ni mtu mzima wa kiume alie fikia umri wa utu uzima.
Mawazo yako yapo sahihi kwa tafasiri ya age ila linapokuja swala la saikolijia utaona kuna wanaume wengi wenye umri mkubwa lakini bado wana mentality ya kivulana.

Hapa inshu ipo kwenye mindset mkuu
 
Mawazo yako yapo sahihi kwa tafasiri ya age ila linapokuja swala la saikolijia utaona kuna wanaume wengi wenye umri mkubwa lakini bado wana mentality ya kivulana.

Hapa inshu ipo kwenye mindset mkuu
Kwa tafsiri yako ya mvulana na mwanaume imelenga namna yaku mtreat mwanamke , ila kwa tafsiri ya mvulana hata umri wa kumiliki mwanamke hajafikia...
 
Hii tafsiri ya mwanaume na mvulana , mara nyingi hutumiwa na wadada wa mjini kuwaseti vijana ili wawe watumwa wao.

Mvulana ni mtoto wa kiume ambae bado hajafikia umri wa utu uzima.

Mwanaume ni mtu mzima wa kiume alie fikia umri wa utu uzima.
Saaafi
 
Back
Top Bottom