Tofauti Kati ya Uwiano na Usawa

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
Naomba mwenye ufafanuzi wa haya maneno anijuze tafadhali
 
uwiano ni kitu/jambo fulani juu ya jambo fulan/kitu=x:y,sawa ni hali yakufanana kwa ukaribu kwa mambo au vitu
 
Mimi nnavyojua usawa ni kufanana au kulingana....ila uwiano ni kuwa sawa kwa kuzingatia tofauti zilizopo (jinsia,umri,elimu n.k)vikwazo au mazingira..
Mfano:
uwiano wa ufaulu kati ya wavulana na wasichana....ina maana tunaangalia uwiano wa kufaulu kwa kuzingatia idadi ya wavulana na wasichana waliofanya mtihani mfano wasichana walikuwa 100 wamefaulu 20 na wavulana 50 wamefaulu 10...hapo uwiano upo sawa..
Mfano mwingine ni kiwango cha uelewa kwa kuzingatia umri....mtoto wa miaka nane hawezi kuwa sawa na kijana wa miaka 20 ila uelewa wao unaweza kuwiana....yan unawalinganisha kwa kuzingatia umri wao.
Mfano mwingine ni majukumu ya mwanamke na mwanaume.....hayafanani lakini yana uzito sawa....kila jukumu lina uzito wake mahali husika....kila mtu akibeba majukumu yake akayafanya kwa asilimia zote uwiano unakuwa sawa....
Sijui nimeeleweka????? Maana usikute maelezo mengi af content sifuri....ila mi nimeelezea ki-ngwiningwini sijui wanamahesabu watasemaje
 
ni kweli kila ukizidi kuzama ndio unapotea
 
bado sijatii kiu lakn asante

Basi tumia tafsiri, peleka kwanza kwenye kiinglish halafu utafute maana yake kwa lugha hiyo ya kiinglish. Kwa kiinglish Uwiano ni ratio na Usawa ni equality.
 
Basi tumia tafsiri, peleka kwanza kwenye kiinglish halafu utafute maana yake kwa lugha hiyo ya kiinglish. Kwa kiinglish Uwiano ni ratio na Usawa ni equality.
SAWA KABISA MASUKE..naanza kukupata........ishushe kwa kiswahili sasa
 
Basi tumia tafsiri, peleka kwanza kwenye kiinglish halafu utafute maana yake kwa lugha hiyo ya kiinglish. Kwa kiinglish Uwiano ni ratio na Usawa ni equality.
inaweza pia kuwa equity and equality? ipi ni ipi hapo Masuke?
 
inaweza pia kuwa equity and equality? ipi ni ipi hapo Masuke?

Kwa Kiswahili inawezekana haya maneno mawili yakawa na tafsiri moja au pengine kila moja lina tafsiri yake hii ni kwa sababu hatujui maneno mengi ya kiswahili ya kitaalamu, lakini maana zake ni tofauti. Mfano: Ukiwa na laki moja na ukaamua kuwagawia watoto watano kila mmoja atapata elfu 20, hiyo ni equality. Na ukiwa na laki moja hiyo hiyo na ukasema nani hana hela hapa kati ya wale watano wakajitokeza watatu wakasema hawana na wengine wakasema wanazo basi ukaamua uwape wasio kuwa nazo hiyo ni Equity. Kwa maana nyingine Equality unagawa kwa sawa kwa kila mtu lakini Equity ni pale wenye uhitaji wa lazima ndo wanaopata au wanapata zaidi.

Uwiano yenyewe ni kugawa kwa ulinganifu kulingana na makundi: Mfano Unaweza kusema kati ya wale watoto watano, wawili ni wa kiume na watatu ni wa kike, na ukaamua kuwagawia kila moja watakayopata wa kiume basi wa kike wapate tatu, hivyo utakachofanya ni kuchukua elfu 25 utawapa wa kiume wagawane na utachukua elfu 75 utawapa wa kike wagawane:
Na uwiano utakuwa hivi; Mgawo wa Watoto wa Kiume kwa ule wa Watoto wa Kike ni Tshs 25,000 kwa Tshs 75,000. ambayo ukiipeleka kihesabu itakuwa; Wa kiume: Wa kike = 1:3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…