Mimi nnavyojua usawa ni kufanana au kulingana....ila uwiano ni kuwa sawa kwa kuzingatia tofauti zilizopo (jinsia,umri,elimu n.k)vikwazo au mazingira..
Mfano:
uwiano wa ufaulu kati ya wavulana na wasichana....ina maana tunaangalia uwiano wa kufaulu kwa kuzingatia idadi ya wavulana na wasichana waliofanya mtihani mfano wasichana walikuwa 100 wamefaulu 20 na wavulana 50 wamefaulu 10...hapo uwiano upo sawa..
Mfano mwingine ni kiwango cha uelewa kwa kuzingatia umri....mtoto wa miaka nane hawezi kuwa sawa na kijana wa miaka 20 ila uelewa wao unaweza kuwiana....yan unawalinganisha kwa kuzingatia umri wao.
Mfano mwingine ni majukumu ya mwanamke na mwanaume.....hayafanani lakini yana uzito sawa....kila jukumu lina uzito wake mahali husika....kila mtu akibeba majukumu yake akayafanya kwa asilimia zote uwiano unakuwa sawa....
Sijui nimeeleweka????? Maana usikute maelezo mengi af content sifuri....ila mi nimeelezea ki-ngwiningwini sijui wanamahesabu watasemaje