Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
Huwa tunasanibisha ama kuchanganya hivi vitu viwili
PEPO ni jina ama ni kiambishi cha kiwakilishi cha hali fulani ikiwa na maana ya kitu chema sana mfano
Kuishi katika pepo ya mahusiano
Kuishi katika pepo ya ukwasi
Kuishi katika pepo ya umaarufu,heshima ,kuabudiwa nk
PEPONI ni mahali dhana pa kufikirika...mahali pazuri penye utimilifu wa vitu vyote vema.. na kwa mazoea ya kiasili ...peponi panafikika tu baada ya kuondoka toka maisha haya yaani kufa lakini hufiki siku hiyo hiyo bali utakaa kaburini mpaka siku ya kiama..siku ya hukumu kuu...matendo yako mema katika utimilifu wake na uchaji wako kwa Mungu wako ndio tiketi ya kukupeleka peponi. Tunapowaombea marehemu wakalale mahali pema peponi sio sasa bali ni siku ya kiama!
Kwa muktadha huu basi pepo kwa maana asili ya msingi inashabihiana na peponi..kwa tafsiri ya uzuri, wema, starehe na raha zote unazojua na usizozijua...hivi viwili ni ukamilifu wa kula bata katika viwango vya juu mno!
Pepo na peponi ni kwa ajili ya kuufurahisha na kuupa ridhiko kuu mwili wa nyama na mwili wa roho...ndio maana huwa tunasikia kuna wenzetu wanaishi pepo ya dunia...kwamba kwa maisha wanayoishi na simulizi tuambiwazo kuhusu peponi basi hawa huanza hayo maisha hata kabla ya kufa
Sasa MAPEPO ninini? Mapepo ni wingi wa pepo...pepo ni umoja...Kama nilivyotangulia kusema kuwa pepo ni dhana dhanifu ya kitu chema basi kuna roho zilizolala kaburini kusubiri kiama ambazo hukengeuka na kutoroka kwenda kuitafuta pepo ya peponi kabla ya kiama.
Ni roho hizi zilizokengeuka ndio hugeuka mapepo ya viwakilishi mbalimbali vya starehe za kidunia na mapepo maarufu sana ni mapepo ya vilevi na ngono, huku pepo kuu likiwa ni ngono kutokana na ile kitu tunaambiwa dhambi ya asili pale Eden
Mapepo hugeuka kadhia kwa wengine kwakuwa yanakupa pepo ya muda tuu na hii ni kutokana na kuwa hawana kibali bado cha kufanya hayo bali ni kama wizi ama kunyapia tu. katika mwili wako wa nyama unaweza kuona kadhia ukishamaliza lakini utataka tena na tena kwakuwa si wewe bali ni pepo
Kwa tafsiri hii ya pepo, tunafichwa mengi kuhusu peponi japo kuna baadhi ya simulizi za kiimani kuwa huko peponi ni bata tu la kula vigoli tupu ...yaani zote ni brand new unavunja mwenyewe.
Je, pepo lako ni lipi? Na linapokuingia si unahisi uko peponi kabisa?[emoji3][emoji3][emoji3]
Good morning Tanganyika!!!