Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,187
Neno Hali ya Hewa (climate) linamaanisha mkusanyiko wa mada (elements) mbalimbali kuu kama: mvua (precipitation); joto (temperature); unyevunyevu (humidity); mawingu (clouds-cover), upepo (winds); mwanga (solar radiation) na atmospheric pressure. Katika vyote hivyo, kiwango cha mvua na joto vina athari kubwa zaidi katika ukuaji wa akili za jamii za wanadamu popote walipo duniani.
Bara la Afrika ndilo lenye joto kali kuliko mabara yote duniani kutokana na Msitari wa Ikweta kupita katikati wa Afrika. Kutokana na joto kali (>23 degree centigrade), maeneo pekee barani Afrika yaliyokuwa na uhakika wa uzalishaji wa chakula ni yale yanayopata mvua nyingi (heavy rainfall >1200) na angalao miezi 9 ya mvua inayofikia mm 100 @ mwezi.
Hata hivyo, maeneo ya milimani (high altitude) hayana joto kali na yanaweza kuwa na uhakika wa chakula kwa kiwango cha mvua chini ya mm 1200 kwa mwaka. Kadri unavyoenda Kaskazini ama Kusini mwa Ncha za Dunia, jotoridi huwa linapungua, hivyo Mashariki ya Kati licha ya kuwa jangwani, ina joto kidogo (<20C) kuliko Afrika huku Ulaya (<16) ikiwa na baridi kuliko Mashariki ya Kati.
Kadri unavyopanda milima (altitudes) na kadri unavyokwenda mbali ya Ikweta (latitudes), ndivyo joto linavyopungua, hivyo mahitaji ya kiwango cha mvua (precipitation) nayo kupungua. Eneo linalopata mm 700 barani Afrika (e.g. Dodoma) halina uhakika wa kuivisha chakula lakini kiwango hicho kinatosha vizuri barani Ulaya.
Kihistoria, hapo awali binadamu wa kwanza (Homo Sapiens) waliishi barani Afrika pekee na walianza kuhamia Asia kati ya miaka 400,000 BC - 60,000 BC. Wakiwa Afrika, walikabiliana na joto kali tofauti na hali ya ubaridi ulioko Asia na Ulaya.
Hivyo walivyohamia huko walianza kutofautiana na wale wa Afrika kutokana na hali ya hewa pamoja na aina za vyakula, matunda, mboga, ndege na wanyama walivyokuwa wakila kila siku.
Kwa kuwa barani Afrika kuna joto jingi (ukitoa maeneo ya milimani), ilipelekea maeneo yaliyokuwa yakikimbiliwa zaidi kuwa yale yenye mvua nyingi na yanayopata mvua ya kutosha kwa miezi isiyopungua miezi 9.
Ndiyo maana maeneo yote nchini yanayopata mvua nyingi za vuli zinazoanza mwezi Septemba/Oktoba, yana jamii za watu wengi ambao ni bright sana kutokana na umuhimu wa mvua hizo za vuli ambazo ni za kupandia.
Wataalamu wanadai mvua za vuli (sept - dec) ni muhimu zaidi kuliko zile nyingi za masika (machi - mei) kwa kuwa ndizo za kulimia na kupandia mazao.
Kwa Tanzania, Wilaya zifuatazo zinapata mvua nyingi (>1200) pamoja na miezi isiyopungua 9 ya mvua za mm 100 @ mwezi.
Sifa nyingine muhimu kwa kusaidia ujenzi wa akili ni:

- Bukoba, Muleba na Misenyi.
- Ukerewe na Ukara.
- Buhigwe
- Tarime na Rorya
- Rombo, Moshi, Vunjo na Hai.
- Arumeru
- Muheza, Mkinga, Lushoto na Korogwe.
- Morogoro.
- Pemba na Unguja.
- Mafia.
- Rungwe, Kyela na Ileje.
Sifa nyingine muhimu kwa kusaidia ujenzi wa akili ni:
- Udongo wenye rutuba.
- Joto la kadri (<21C) ili mwili kutopoteza nishati nyingi kupitia kuchomwa na miale ya jua.
- Kutokuwepo kwa Ugonjwa wa Malaria na Homa ya Manjano (Yellow Fever).
- Kutokuwepo kwa Ugonjwa wa Malale (Sleeping Sickness/Trypanasomiasis/Nagana).
- Kutokuwepo kwa Ugonjwa wa Kichocho (bilharzia/Schistosomiasis).
- Kutokuwepo kwa kiwango kikubwa cha Fluoride (<1.5 mg/L) kwenye vyanzo vya maji.
- Uwepo utajiri wa Samaki hasa wa maji baridi.
- Uwepo utajiri wa Mifugo hasa ng'ombe wa maziwa kwa ajili ya nyama na maziwa
- Uwepo wa Madini ya Iodine.