Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Mwenye macho haambiwi tazama.
Kuna mikutano miwili. Wa CCM Dodoma na hii ya uchaguzi wa CHADEMA wakipanga safu yao ya uongozi.
Kwa upande wa CCM tunaona hakuna hoja za msingi kuufanya mkutano wao uwe na mvuto zaidi ya show off ya mabasi, mabango kila sehemu huko Dodoma na matumizi ya wasanii ambavyo kwa kifupi vyote ni matumizi mabaya ya kodi za wajinga wa Tanzania.
Ila upande wa CHADEMA tunaona malumbano ya hoja za msingi na mchakato wa uchaguzi ulio wazi wa kidemokrasia ukiwavutia watanzania kufuatilia kwa karibu mikutano inayoendelea ya chama hiki.
Watanzania wanapata nafasi ya kujua wagombea wa Chadema, sera zao, maono yao na wakishuhudia midahalo ya Timu zao za Kampeni. Vyote hivi vinafanyika kwa kupigana vijembe kweli huku chama hiki kikiendelea kuwa kimoja bila kuvunjika tofauti na matarajio ya wapiga ramli wa CCM.
Kweli kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza.