Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kwa ufahamu tu:
Tofauti kati ya Daftari la Kudumu la Wapigakura na Daftari la Wapigakura wa Serikali za Mitaa
Daftari la Kudumu linasimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi kwa ajili ya Kumchagua Diwani, Mbunge na Rais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
Daftari la Wapigakura wa Serikali za Mitaa linasimamiwa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI na ni kwa ajili ya Uchaguzi wa Wenyeviti wa Vijiji, Wajumbe, Wenyeviti wa Vitongoji na Wenyeviti wa Mitaa.
Daftari la Wapigakura wa Serikali za Mitaa litaanza kuandikishwa kuanzia tarehe 11 - 20/10/2024
Uandikishaji utafanyika kwenye Ofisi Vitongoji na Mitaa au kwenye Majengo ya Umma ya maeneo hayo na vituo vitafunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na mbili Jioni
Zoezi hili ni kwa Tanzania Bara na litafanyika kwa muda wa siku 10.
NB: Kila mtu anajiandikisha katika eneo analoishi yaani Kitongoji/Mtaa wake.
Chanzo: TAMISEMI
Pia soma ~ Rais Samia kuzindua uandikishaji wa Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa Oktoba 11, 2024 - Dodoma