Uchaguzi 2020 Tofauti ya Ilani (CHADEMA vs CCM) katika uchaguzi wa 2020

Uchaguzi 2020 Tofauti ya Ilani (CHADEMA vs CCM) katika uchaguzi wa 2020

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,206
Reaction score
18,549
TOFAUTI YA ILANI YA CCM NA ILANI YA CHADEMA UCHAGUZI WA 2020.

1. Ilani ya CCM haizungumzii kupunguza Kodi wakati ilani ya CHADEMA inalenga kupunguza Kodi ya ongezeko la thamani ili iendane na nchi jirani na kuondoa utitiri wa kodi (multiple taxation)

2. Ilani ya CCM haizungumzii kuongeza mishahara wala kufidia nyongeza ambazo watumishi walipunjwa miaka mitano iliyopita wakati CDM inategemea kuleta bajeti za ziada kufidia nyongeza mishahara ya miaka mitano ambayo watumishi hawakupata nyongeza ya mishahara wala kupanda madaraja.

3. Ilani CCM haizungumzii kupunguza marejesho ya mikopo ya elimu ya juu(HELSB) wakati CDM inategemea kuweka marejesho ya asulimia 3 kwa wahitimu wa vyuo vikuu badala ya asilimia 15 ya Sasa ambayo iliongezwa kinyume na mkataba wa mkopo kwa kufanya marekebisho ya sheria ya Sasa na kwamba mhitimu alipe baada ya kupata kazi.

4. Ilani ya CCM haizungumzii agenda ya Katiba Mpya wakati ile ya CHADEMA inazungumzia kurudisha mchakato wa katiba mpya ulioasisiwa na jaji Warioba ndani ya siku mia za Kwanza.

5. CCM inaamini kwenye maendeleo ya vitu wakati CHADEMA inaamini katika maendeleo ya watu zaidi. Yaani maisha yawatu ndio yawe bora zaidi badala ya vitu Kama ndege.

6. Ilani ya CCM haizungumzii kulinda uhuru wa habari Kama kipau mbele wakati ilani ya CHADEMA inaweka kipaumbele mojawapo ni kurejesha Uhuru wa habari.

7. Ilani ya CCM haizungumzii kugatua madaraka na kufanya wananchi wawe na nguvu zaidi ya kuamua mambo yao wakati ilani ya CHADEMA inapendekeza kupeleka nguvu zaidi kwa wananchi.

8. Ilani ya CCM haitoi mkazo wa uchumi kumilikiwa na sekta binafsi( wananchi) bali serikali wakati ilani ya CHADEMA inaweka kipaumbele uchumi wa watu( sekta binafsi)

9. Ilani ya CCM haizungumzii bima ya afya kwa watu wote wakati ilani ya CHADEMA inataka watu wote wawe na bima ya afya.

10. Ilani ya CCM inazungumzia kudumisha Muungano was serikali mbili wakati Ilani ya CHADEMA inazungumzia Muungano wa serikali tatu zilizopendekezwa na wananchi kwenye tume ya Jaji Warioba.

11. Ilani ya CCM haizungumzii kuondoa Kodi kwenye maduka ya majeshi ya Polisi, jeshi la wananchi, magereza na Zimamoto Kama hapo awali ili kuwapa wanajeshi unafuu wa maisha wakati CHADEMA inapendekeza kurejesha unafuu huo.

12. Ilani ya CCM haizungumzii marudhiano ya kitaifa wakati ilani ya CHADEMA inapendekeza kuleta maridhiano ya kitaifa ndani ya siku mia za Kwanza.

13. Ilani ya CCM haizungumzii kufuta sheria kandamizi wakati ilani ya CHADEMA inapendekeza kufuta sheria zote kandamizi.

IMG-20200831-WA0029.jpeg
IMG-20200831-WA0030.jpeg
 
Haya mambo hayawafikii wananchi vyema ndio maana wanakengeuka kukichagua hicho chama chakavu!
 
Ilani ya CHADEMA imejaa kujaza pesa watu mifukoni lakini inashindwa kuonyesha upanuzi wa huduma kwa wananchi. Hakuna hospitali mpya, shule mpya, vyuo vipya wala miradi mipya ya kimaendeleo.

Hii ni kama kurudi nyuma miaka ya 70 na 80, ambapo watu walikuwa na fedha nyingi wanaficha kwenye soksi lakini inabidi watebee mji mzima kutafuta kipande cha sabuni.
 
Ilani ya CHADEMA imejaa kujaza pesa watu mifukoni lakini inashindwa kuonyesha upanuzi wa huduma kwa wananchi. Hakuna hospitali mpya, shule mpya, vyuo vipya wala miradi mipya ya kimaendeleo...
Mkuu bado tuhahitaji mill 50 za kila Kijiji.
 
Mkuu bado tuhahitaji mill 50 za kila Kijiji.
Kwani uliambiwa vijiji vitadhikiswa fedha taslimu mkononi? Mbona mnafumbia macho huduma zilizosogezwa karibu kabisa na wananchi vijijini? Umeme, majini, vutuo vya afya, masoko, barabara nk.
 
Kwani uliambiwa vijiji vitadhikiswa fedha taslimu mkononi? Mbona mnafumbia macho huduma zilizosogezwa karibu kabisa na wananchi vijijini? Umeme, majini, vutuo vya afya, masoko, barabara nk.
Kwahio hizo huduma gharama yake ni mill 50 kila Kijiji?. Hizo umeme,maji,vituo vya afya na n.k vyote aliahidi, lakini bado tuhahitaji mill 50 za kila Kijiji.
 
Kwahio hizo huduma gharama yake ni mill 50 kila Kijiji?. Hizo umeme,maji,vituo vya afya na n.k vyote aliahidi, lakini bado tuhahitaji mill 50 za kila Kijiji.
Hizo huduma ni maradufu ya milioni 50.

Vijiji vyote vina wabunge wao na wengine ni CHADEMA, kwanini wameshindwa kudai hiyo million 50. Ni kwasababu wote walisha elimishwa nini maana ya milioni 50. Kama unabishamuulize mbunge wako waliyemaliza muda wake.
 
Kiujumla ccm imechoookaa mpaka haijiamini inakimbilia ushindi wa mezani halafu unajitapa kiongozi wa wananchi uliona wapiii!? ulisikia wapi!? Ulichaguliwa wapi!?
 
Back
Top Bottom