Tofauti ya Kibaka, Mwizi na Jambazi

Tofauti ya Kibaka, Mwizi na Jambazi

Jaylee

Member
Joined
Apr 15, 2009
Posts
66
Reaction score
96
Naomba kufahamu tofauti baina ya Kibaka, Mwizi na Jambazi.

Je ni lini Kibaka anakuwa Mwizi au kinyume chake?
Na je ni lini Mwizi anaitwa Jambazi au kinyume chake?

Ni mazingira gani yanamfanya mhalifu kuitwa Kibaka au Mwizi au Jambazi?

Nawasilisha
 
Kibaka anaishi maisha ya hovyo, ni maskini.

Mwizi anaiba na kuumiza kwa silaha na hutamjua.

Jambazi anakuja kuchua mali yako kama yake. Hakuumizi na ikiwezekana ni mtu unamjua kabisa.
 
Kibaka anaiba kwa kukaba halafu anakimbia ni rahisi kumkamata kibaka...mwizi ni mtu mwenye tabia ya wizi akiishaiba anakimbia kwa speed kali huwezi kumkamata kama wewe sio mwizi..jambazi ni mtu anaepiga matukio makubwa na anakuwa amejipanga kwerikweri akiishaiba anakuwa na usafiri wa pikipiki au gari.....kule jera kuna msemo wale wafungwa huwa wanaambizana kwamba kimbia kama siku ulivyopiga tukio"...
 
Kibaka anaishi maisha ya hovyo, ni maskini.

Mwizi anaiba na kuumiza kwa silaha na hutamjua.

Jambazi anakuja kuchua mali yako kama yake. Hakuumizi na ikiwezekana ni mtu unamjua kabisa.
Nakupa 0.1/10

iyo nayo nikwa mwandiko mzuri
 
Kibaka ni mkwapuaji wa vitu vidogo vidogo. Hutumia zaidi nguvu

Mwizi anatumia akili na nguvu Ili wakati anakuibia usimshtukie, uje ujue huko mbele ya safari. Hapa pia ndo Kuna kundi la matapeli, wao wanacheza na maneno au kalamu (forgery).

Jambazi hutumia zaidi silaha. Bunduki, sime, mawe.....

Kwa uhakika zaidi tembelea TUKI
 
Kibaka huiba vitu vidogo vidogo Kama simu, nguo, viatu etc. Kibaka hapangi, hajui ataiba nini kesho. Wengi utawakuta gerezani.
Jambazi hupanga matukio kabla, jambazi hutumia nguvu kuiba na anakuibia unaona na usipokua mpole anakumaliza. Wengi wako magerezani au polisi huwamaliza kwa RISASI. Jambazi Hana urafiki na polisi.
Mwizi....wengi wao ni wafanyakazi wa serikali, Mara nyingi wanamuibia mwajiri wao (serikali) wezi hawafanywi chochote na huwezi kuwakuta jela. Akishaiba idara Fulani anahamishiwa idara nyingine akaibe vizuri. Wengi wa wezi ni watu waheshimiwa Sana kwenye jamii yetu.
Mwizi usipomuita mheshimiwa anaweza kukuchulia hatu.
 
Jambazi aibi, hupora kwa kutumia silaha..tukio la ujambazi lipo organised, mpaka anakuja ana taarifa zote na atatumia dakika ngapi..jambazi ana mtaji..
 
Kibaka hapangi tukio....anaamka asubuhi anaaga anaenda kazini..bila kujua atapiga tukio wapi,kwa nani wala muda gani...anaweza toka geto kwake anapiga hatua mbili na wewe umejipitisha hapo.basi show inaishia hapo hapo..

Mwizi anapanga tukio kwa kumsoma mhusika wake.anajua una nini cha kukuibia,unavilinda kwa staili gani,lini au muda gani utakuwa wapi ili akutaimu vizuri...MWIZI HAPENDI KUJULIKANA...ndio maana anapenda kuiba usiku au sehemu pweke kwa tahadhali kubwa.hatumii silaha za moto zaidi ya vitendea kazi vyake

Kaka jambazi..yeye ni kama mwizi kidogo..kwan analipanga tukio kwa ustadi mkubwa..anajua atachukua mali gani...atachukua kwa nani na atakimbilia wapi..JAMBAZI anafanya tukio live..japo anaweza kuficha sura lakini ni tukio ambalo linafanyika bila kificho..ndio maana wanakuwa na silaha za moto ili kiwatisha watu wasisogelee au kuharibu mpango wao..

Tapeli ni yule anakuibia kwa kukulaghai..yaani ni wewe mwenyewe unajikuta unampa mali zako na baadae kugundua kwamba haikupaswa ufanye hivo..mara nyingi wanatumia mitandao,lugha nyepesi na sometimes uchawi au madawa
 
Kwenye huu uzi utajua vibaka,wezi na majambazi!.. fatilieni tu watu wanavyojibu kazi zao kama essay vile..😂
 
Kibaka ndio anaangukiaga mikononi mwa wenye nchi yao wakiwa na hasira fasta anatembezewa kichapo na akipona ndio anakua amegraduate kwenda kua mwizi..[emoji559][emoji559][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom